Trudeau aliingia madarakani mwaka 2015, miaka kumi baada ya utawala wa chama cha Consrvative, akijozoelea sifa kwa jitihada zake za kuirudisha Canada katika enzi yake ya liberali./Picha: Wengine         

Akizungumza siku ya Jumatatu, Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, amemuomba Rais wa Chama Cha Liberal cha nchini humo kuanza mchakato wa kumtafuta mbadala wake.

"Nina nia ya kujiuzulu nafasi ya Uwaziri Mkuu na kiongozi wa chama,” alisema Trudeau ambaye amekuwepo madarakani toka mwaka 2015 katika mkutano wake na waandishi wa habari.

Kabla ya kutoa tamko hilo la kujiuzulu, chanzo kimoja kilidokeza kuwa Bunge la nchi hiyo litaahirishwa hadi Machi 24, licha ya kupangwa kuanza tena Januari 27.

Muda huo unatarajiwa kutoa nafasi kwa chama cha Liberal kufanya uchaguzi wa viongozi wa chama hicho.

Wakati akitangaza nia yake, Trudeau alisisitiza kuwa “vita vya ndani ya chama cha Liberal” ni ishara kuwa yeye “si mtu sahihi katika uchaguzi ujao”.

Utawala wa Trudeau, ambaye amekuwepo madarakani tangu mwaka 2015, umekumbwa na ‘sintofahamu’ inayotokana na kukosekana kwa imani juu ya uongozi wake, hasa baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri wa Fedha wa nchi hiyo, Chrystia Freeland mwaka 2024.

Trudeau aliingia madarakani mwaka 2015, miaka kumi baada ya utawala wa chama cha Consrvative, akijozoelea sifa kwa jitihada zake za kuirudisha Canada katika enzi yake ya liberali.

Hata hivyo, kiongozi huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa kuwa mmoja Waziri Wakuu maarufu wa nchi hiyo Pierre Trudeau, alianza kupoteza umaarufu miongoni mwa wapiga kura kutokana na sababu kadhaa, ikiwemo ongezeko kubwa la bei za vyakula na makazi.

TRT Afrika