Urusi yaripoti mashambulizi  ya ndege zisizo na rubani yaliyojiri usiku kucha

Urusi yaripoti mashambulizi  ya ndege zisizo na rubani yaliyojiri usiku kucha

Wakuu wa Kursk, eneo la Smolensk wanadai ndege kadhaa zisizo na rubani za Kiukreni zilidunguliwa Alhamisi usiku
Ndege mbili zisizo na rubani ambazo ni za masafa marefu zilishambulia  miundombinu ya nishati. Picha AA

Maafisa wa Urusi siku ya Ijumaa waliripoti mashambulizi mengi ya ndege zisizo na rubani katika mikoa, inayopakana na Ukraine, iliyotekelezwa Alhamisi usiku, shirika la anodolu linaripoti

Gavana wa eneo la Kursk nchini Urusi, Roman Starovoit, alisema katika taarifa yake kwenye Telegram kwamba "ndege kadhaa zisizo na rubani za Ukraine zilidunguliwa" karibu na kituo cha utawala cha eneo hilo, mji wa Kursk.

Starovoit alitoa wito kwa wananchi kuwa watulivu na kuripoti matokeo ya vitu vyovyote vinavyotiliwa shaka, ikiwa ni pamoja na magari ya anga.

Kando, gavana wa mkoa wa Smolensk, Vasily Anokhin, alisema kwenye Telegraph kwamba magari mawili ya angani ya masafa marefu ambayo hayana rubani yalishambulia vitu vya miundombinu ya nishati.

"Hakuna majeruhi, uharibifu mkubwa, au moto," Anokhin alibainisha.

Vikosi vya jeshi la Ukraine vimeripotiwa kufyatua mfululizo wa mashambulizi katika maeneo ya mpakani mwa Urusi katika miezi ya hivi karibuni, hususan Bryansk na Belgorod, ambayo yalipigwa na ndege zisizo na rubani na mizinga, kulingana na Moscow.

AA