Vita hivyo vilisababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000, takriban asilimia 70 wakiwa Wabosnia / Picha: AA.

Akiwa anaishi mbali na maeneo ya mauaji ya Bosnia wakati wa kilele cha vita vya 1992-95, Semiha Bahadir alikuwa akipambana na hasara ya kibinafsi - alimpoteza mtoto wake wa miaka mitatu katika ajali mwaka 1993 - mbali na kushiriki uchungu wa Wabosnia wenzake. .

Akiwa ameolewa na kuishi Istanbul, Bahadir alipata habari hizo kutoka nchi yake kwa masikitiko makubwa.

Akiwa mtaalamu wa tabia, alifunzwa kukabiliana na maumivu na kiwewe kwa kuelewa na kuchanganua tabia za binadamu, hasa katika muktadha wa saikolojia na mwingiliano wa kijamii.

Lakini hakuna chochote maishani ambacho kingeweza kumuandaa kukabiliana na ukatili wa wavamizi hao pale maelezo ya kutisha yalipoibuka kuhusu mauaji ya halaiki ya Srebrenica - wakati vikosi vya Waserbia vilipowaua zaidi ya wanaume na wavulana 8,000 wa Kiislamu baada ya kuuvamia mji huo Julai 11, 1995, katika hatua za mwisho za vita.

Kumbukumbu ya Mauaji ya Kimbari ya Srebrenica huko Potocari Picha : Reuters

Katika mkesha wa maadhimisho ya miaka 28 ya mauaji ya halaiki - yaliyorekodiwa kama ukatili mbaya zaidi tangu Vita vya Pili vya Dunia - Bahadir anafichua maelezo ya kutisha ya ukatili waliofanyiwa Waislamu wa Bosnia, akipigi amfano historia yake ya kipekee na kubadilishana maarifa aliyopata kutokana na mwingiliano wake na manusura.

"Ninafungua roho kuhusu Srebrenica kwa mara ya kwanza kabisa…Imekuwa mlango uliofungwa ndani yangu kwa zaidi ya miaka 20," anasema Bahadir, ambaye sasa ana umri wa miaka 57.

mauaji ya kimbari ya Bosnia

Anakumbuka jinsi alivyoanza safari ya uponyaji na mabadiliko.

"Maumivu makali kutoka ndani na nje yaliniacha nikijiuliza jinsi ya kukabiliana nayo," alikumbuka Bahadir, sauti yake ikijaa tafakari ya kina. "Hivi karibuni nilitambua kwamba kusonga mbele na kurudi kwenye maisha ya 'kawaida' haikuwezekana mbele ya maumivu hayo makubwa. Iliniongoza kutafakari upya swali: ninawezaje kujifunza kuishi na maumivu haya?"

Kwa kutumia ujuzi wake, alitafuta kitulizo katika kuelewa kina cha uthabiti wa mwanadamu.

Dhamira ya Bahadir ikawa wazi: kuwasaidia watu wake kupata nguvu katikati ya dhiki, kurejesha utambulisho wao, na kujenga upya maisha yao.

Hizi ni hadithi za Wabosnia ambao waliona mabaya zaidi ya ubinadamu na wakanusurika kusimulia hadithi zao.

‘Waambie ili tueleweke’

Katika wakati muhimu wakati wa vita, Alija Izetbegovic - rais wa kwanza wa Bosnia na Herzegovina na kuheshimiwa kama 'mfalme mwenye busara' - aliwasiliana na mke wake Halida, ambaye wakati huo alikuwa akiishi Istanbul baada ya kuhamishwa kutoka nchi iliyoharibiwa na vita.

Halida Izetbegovic na Alija Izetbegovic kwenye mitaa ya Sarajevo Picah : AA

Wakati huo, Bahadir alisimama karibu na Halida Izetbegovic kama mshauri na mkalimani wake kwa zaidi ya miaka 6, na kujenga uhusiano wa karibu na wa kudumu kati yao.

Bahadir anamkumbuka Halida Izetbegovic akimweleza kuhusu maneno ya Alija Izetbegovic yenye hisia kali kwenye simu alipompigia: “Waambie, ili tueleweke.”

Alimuelekeza mke wake kumulika kw aulimwengu mzozo wa kibinadamu unaojitokeza katika nchi yake na eneo zima la Balkan.

Alija Izetbovic akiwa na familia yake Picha : AA

Halida Izetbegovic na Semiha Bahadir waliandaa mkutano katika Chuo Kikuu cha Marmara, kwa lengo la kuwatambulisha watu wa Bosnia na kutoa ufahamu katika michakato ya kihistoria na kitamaduni ya Balkan.

Mkutano huo uliwaleta pamoja watu kutoka makabila mbalimbali, na kuwashangaza Izetbegovic na Bahadir.

"Mateso hayana lugha, dini, rangi, au wakati," Bahadir anaiambia TRT World, akimaanisha kuungwa mkono kwa Wabosnia wakati wa mkutano huo.

Mwili uliotenganishwa na roho

Bahadir anakumbuka alikutana na msichana wa Bosnia mwenye umri wa miaka sita ambaye alishuhudia kuuawa kwa mama yake, nyanyake, na wanafamilia wengine wa kike mikononi mwa askari wa Serbia.

Msichana huyo - ambaye utambulisho wake umebanwa ili kulinda usiri wake - alifichwa na familia yake kwenye pipa wakati wanajeshi wa Serb walipovamia nyumba yao. Baba yake, babu, na jamaa wengine wa kiume wa familia walitolewa nje ya nyumba na hawakuonekana tena.

Akiwa ameokolewa na kufikishwa katika kambi ya wakimbizi ya Kituruki, alipata faraja chini ya uangalizi wa tabibu wake, Bahadir.

"Ilikuwa ya kwanza katika taaluma yangu," Bahadir anasema. "Kulikuwa na mwili na roho iliyovunjika, lakini hatukuona maelewano yakiyafunga haya mawili."

Kutokana na dhamira isiyoyumba ya Bahadir, safari ya uponyaji ya msichana iliendelea.

"Niliona ni vitu ngapi maalum na vya kupendeza ambavyo vinaweza kutokea kutoka kwa shida kama hiyo," anasema. "Msichana huyu mdogo hatimaye alipona, alianza kuzungumza lugha saba kwa ufasaha akiwa na umri wa miaka 16, na sasa, anafanikiwa kama sauti yenye ushawishi kwenye majukwaa ya kimataifa."

‘Mungu alichukua 17, lakini alitupatia 70,000’

"Nena", kumaanisha bibi katika lugha ya Kibosnia, anachukuliwa kuwa kiini cha familia na anapewa heshima kubwa katika jamii ya Bosnia.

"Maumivu ni kichocheo cha mabadiliko ya kijamii na kimataifa na yalikuwa na siku zijazo zilizojaa mwanga, utulivu na ukomavu." Picha : AA

Wakati wa vita vya Bosnia, nena mmoja aliuteka moyo wa Bahadir katikati ya machafuko. Licha ya kupoteza wanafamilia 17, mama huyo mwenye umri wa miaka 85 aliwatia moyo wote kwa nguvu zake zisizoweza kuyumba. Akiwa na mjukuu mmoja tu aliyesalia akitafuta kimbilio huko Uturuki, alidumisha tumaini na shukrani kwa Mungu.

Wakati wa ziara ya moja ya kambi za wakimbizi, Bahadir alikuwa na mwingiliano wa kukumbukwa na Nena.

"Kwa nini wanawake hawa wamechoka sana?" ajuza huyo aliuliza, akimaanisha wanawake wengine wa Bosnia katika kambi.

Bahadir anakataa kuyaita mauaji ya halaiki 'vita', neno rasmi linalotumika kwa ghasia zilizofanywa kwa Waislamu wa Bosnia. “Kuita kilichotokea Bosnia kuwa vita ni dhuluma kwa Wabosnia; kunapaswa kuwa na usawa wa nguvu katika vita."

Anasisitiza hoja yake kwa kuonyesha jinsi Waserbia walitumia ubakaji kama silaha ya vita na jinsi wanawake hawakuruhusiwa kutoa mimba katika jaribio la utaratibu la Waserbia kuleta usumbufu kati ya vizazi vya Waislamu wa Bosnia.

Kupitia ukatili huo, vile “vipimo vitano vya kujiokoa ”—usalama wa maisha, akili, mali, uzao, na uhuru wa imani—zililengwa kikatili wakati wa vita vya Bosnia, na kuharibu kila nyanja ya uhai wa binadamu.

Bahadir anaangazia hitaji la habari sahihi na ufahamu wa pamoja. Kusahau ukatili wa zamani huwaacha wahalifu wakosaji na kuhimiza vurugu za siku zijazo.

Bahadir anarejea onyo la marehemu babu yake, "Tukisahau, tutaendelea kuuawa kila baada ya miaka 50."

Anasema maneno yake yanaendana na hisia za marehemu Alija Izetbegovic, ambaye aliwahi kutahadharisha, "Chochote unachofanya, usisahau mauaji ya kimbari. Kwa sababu mauaji ya kimbari yaliyosahaulika yanarudiwa.

TRT Afrika