Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi na mwenzake wa Irani Ebrahim Raisi mnamo Jumamosi walijadili masuala muhimu kati ya nchi hizo mbili. Picha: Maktaba

Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sisi na mwenzake wa Irani Ebrahim Raisi mnamo Jumamosi walijadili masuala muhimu kati ya nchi hizo mbili na hali ya hivi karibuni katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambao umekuwa chini ya mabomu makali ya Israeli kwa zaidi ya miezi miwili.

Al-Sisi na Raisi walizungumza kwa njia ya simu kuhusu hali ya Gaza pamoja na masuala ya nchi mbili hizo, hayo ni kulingana na taarifa kutoka kwa ikulu ya Misri.

Mawasiliano ya hivi karibuni kati ya nchi mbili hizo yanaonekana kuwa na ufanisi baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri Sameh Shoukry kukutana na mwenzake wa Irani Hossein Amir-Abdollahian mjini New York mnamo Septemba 21, ambapo wanadiplomasia hao wawili wa juu walijadili mahusiano ya nchi zao mbili na njia za kuyaendeleza "kwa njia ambayo hutumikia maslahi ya watu wote (wa nchi)."

Hatua zinazohitajika

Mapema mwezi Mei, Raisi aliielekeza Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi yake kuchukua "hatua muhimu" ili kuboresha uhusiano na Misri, limeripoti Shirika la Habari la Iran Tasnim.

Uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ulikatwa mnamo 1980 kutokana na mafanikio ya mapinduzi ya Iran na shah Mohammad Reza Pahlavi aliyeondolewa kutafuta kimbilio Cairo.

Kuzorota kwa uhusiano kati yao kuliendelea baada ya mkataba wa Camp David kati ya Misri na Israeli.

Hata hivyo mahusiano yao yalirejea tena mnamo 1991 katika ngazi ya ubalozi na sehemu za maslahi.

AA