Bosnia na Herzegovina zinaadhimisha kumbukumbu ya miaka 28 ya mauaji ya kimbari ya Srebrenica ambapo maelfu ya Waislamu wa Bosnia waliuawa.
Mauaji ya Waserbia Mashariki mwa Bosnia na Herzegovina mwaka 1995 yaliua zaidi ya Waislamu 8,000 wa Bosnia, wengi wao wakiwa wavulana na wanaume.
Mauaji ya halaiki ya Srebrenica yaliwaacha wanawake na wasichana wakiomboleza msiba mkubwa zaidi kwao ambayo ni mauaji makubwa ya kimbari barani Ulaya tangu vita vya pili vya dunia.
Waliouawa walitupwa kwenye makaburi ya halaiki yaliyotapakaa eneo la Srebrenica.
Kila mwaka mnamo Julai 11, waathiriwa wapya wanaotambuliwa kuwa waliathiriwa na mauaji haya ya kimbari huzikwa kwenye makaburi ya kumbukumbu huko Potocari
TRT Afrika