Marekani imepinga azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilitaka "kusitishwa kwa vita kwa sababu za kibinadamu" ili kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia na kuokoa maisha kwa mamilioni huko Gaza.
Mswada huo uliwasilishwa na Brazil.
Hata hivyo, Marekani imepinga kwa kutumia nguvu ya kura ya turufu, ambayo mjumbe yoyote katika ya wajumbe wa tano wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ana uwezo wa kuitumia kuzuia pendekezo lolote kupita.
Nchi 15 wanachama zilipiga kura na 12 zikaunga mkono pendekezo hilo.
Nchi hizo ni Albania, Brazili, Uchina, Ekuador, Ufaransa, Gabon, Ghana, Japan, Malta, Msumbiji, Uswizi, na United Arab Emirates, UAE.
Marekani ndiyo nchi pekee ambayo ilipinga pendekezo hili.
Urusi na Uingereza ziliamua kutounga mkono au kupinga mswada.
Nchi tano zina nafasi ya kudumu katika baraza la Amani na Usalama la umoja wa mataifa : Marekani, China, Uingereza, Urusi na Ufaransa.
Mswada wa Urusi waanguka
Tarehe 16 Oktoba baraza la Usalama lilishindwa kupitisha azimio lililotolewa na Urusi ambalo lingetaka kusitishwa mara moja kwa mapigano ya kibinadamu katika mgogoro unaoendelea kati ya Israel na Palestina.
Mswada huu ungelaani vikali ghasia na uhasama unaoelekezwa dhidi ya raia na vitendo vyote vya kigaidi.
Nchi tano ziliunda mswada huo- China, Gabon, Mozambique, Russia, na United Arab Emirates.
Nchi nne zilipinga (France, Japan, Uingereza na Marekani).
wanachama sita hawakupiga kura - Albania, Brazil, Ecuador, Ghana, Malta, na Switzerland.
Kwa masharti yake zaidi, ingetaka pia kuachiliwa kwa usalama kwa mateka wote na utoaji na usambazaji usiozuiliwa wa misaada ya kibinadamu, ikiwa ni pamoja na chakula, mafuta na matibabu.
Ili Baraza lipitishe azimio, pendekezo lazima ingepokea angalau kura tisa za kuunga mkono, na hakuna hata mmoja wa wajumbe wake watano wa kudumu ambaye anapinga au kupiga kura ya turufu.