Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani amesema Alhamisi kwamba mgogoro wa Mashariki ya Kati ni "mauaji ya halaiki ya jumla"/ Picha: AFP  

Kiongozi wa Qatar Sheikh Tamim bin Hamad Al-Thani amesema siku ya Alhamisi kwamba mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati ni 'mauaji ya halaiki ya jumla' na kwamba nchi yake siku zote imekuwa ikionya kuhusu 'mauji' ya Israeli.

"Imekuwa wazi kwamba kinachotokea ni mauaji ya halaiki, na kuifanya Gaza kuwa eneo lisiloweza kukaliwa na binadamu, kuandaa mazingira ya wahamiaji," amesema wakati wa mkutano wa Ushirikiano wa Asia uliofanyika Doha.

Zaidi ya Wapalestina 41,500 waliopo Gaza wameuliwa katika mashambulizi ya Israeli katika eneo hilo lililozingirwa tangu Oktoba 7, kwa mujibu wa mamlaka ya afya katika eneo linaloendeshwa na Hamas.

Wiki hii, Israeli ilianzisha mashambulizi ya ardhini nchini Lebanon dhidi ya Hezbollah inayoungwa mkono na Iran, ambayo imekuwa ikirusha makombora Israeli katika kile inachosema kuonyesha mshikamano na Palestina.

TRT World