Ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu imepokea orodha ya mateka wa Israel wanaotarajiwa kuachiliwa Jumapili katika kundi la tatu la makubaliano ya kubadilishana wafungwa na kundi la muqawama wa Palestina, Hamas, kulingana na ripoti za vyombo vya habari.
Gazeti la Haaretz lilibaini kuwa habari hiyo iliwasilishwa kwa familia za wafungwa waliopangwa kuachiliwa.
Mamlaka za usalama za Israel kwa sasa zinakagua orodha ya mateka, kulingana na gazeti la Yedioth Ahronoth.
Kusitishwa mapigano kwa siku nne kwa maslahi ya misaada ya kibinadamu iliyosimamiwa na Qatar kulianza Ijumaa ambayo ilisimamisha kwa muda mashambulizi ya Israeli dhidi ya Gaza.
Israel na Hamas wamebadilishana Waisraeli 41 wakiwemo raia wa kiwageni na Wapalestina 78 kutoka jela za Israel katika makundi mawili ya kubadilishana wafungwa uliofanywa katika siku mbili za kwanza za kusitisha kwa siku nne za kibinadamu.
Chini ya makubaliano hayo, mateka na wafungwa wataachiliwa kwa makundi katika muda wa siku nne.
Israel ilianzisha kampeni kubwa ya kijeshi huko Gaza kufuatia operesheni ya kuvuka mpaka ya Hamas mnamo Oktoba 7.
Tangu wakati huo Israel imeua Wapalestina 14,854, wakiwemo watoto 6,150 na zaidi ya wanawake 4,000, kulingana na mamlaka ya afya katika eneo hilo.
Idadi rasmi ya vifo vya Israeli inasimama 1,200.