Shirika la la kijasusi la marekani FBI limetoa onyo kwa mara nyingine juu ya utumiaji wa mfumo wa USB wa kuchajia simu uliowekwa katika maeneo ya uma.
Kupitia ukurasa wake wa Twitter taasisi hiyo imechapisha onyo hilo kuwa wadukuzi wanatumia vifaa hivyo vilivyofungwa katika maeneo ya umma ili kuiba taarifa za watu.
"Epuka kutumia vituo vya kuchajia bila malipo katika viwanja vya ndege, hoteli au vituo vya ununuzi. Watu wenye nis mbaya wamegundua njia za kutumia milango ya USB ya umma kutambulisha programu hasidi na ufuatiliaji wa programu kwenye vifaa. Beba chaja yako mwenyewe na kebo ya USB na utumie plagi ya umeme badala yake". chapicho hilo liliandikwa.
Taarifa hiyo haikubainisha matukio yoyote ya hivi majuzi ya madhara ya watumiaji kutokana na udukuzi. Ofisi ya FBI ya Denver ilisema ujumbe huo ulikusudiwa kama ushauri, na kwamba hakuna kesi maalum ambayo ilisababisha.
Vifaa vya watumiaji walio na kebo za USB zilizo athiriwa vinaweza kuchunguzwa kupitia programu ambayo inaweza kuondoa majina ya watumiaji na maneno ya siri.