Erdogan pia atazuru Erbil, Kaskazini mwa Iraq baada ya mazungumzo Baghdad. / Picha: AA

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan amekutana na mwenzake wa Iraq Abdul Latif Rashid kwenye ziara rasmi katika mji mkuu wa nchi Jirani, Baghdad.

"Rais Recep Tayyip Erdogan, ambaye yuko Baghdad kwa ziara rasmi, alikutana Na Rais Abdul Latif Rashid Wa Iraq," taarifa ya kurugenzi ya mawasiliano ya Uturuki imesema.

Katika mkutano huo, uhusiano wa nchi mbili ya Uturuki na Iraq, vita vya Israeli dhidi ya Gaza, masuala ya kikanda na kimataifa, na juhudi za kupambana na ugaidi zilijadiliwa.

Rais Erdogan alielezea matarajio ya Uturuki kutoka Iraq katika kupambana na kundi la kigaidi la PKK na kusisitiza hitaji la Iraq kusafishwa kwa aina zote za ugaidi.

Pia alisisitiza umuhimu wa kurejesha uhusiano kati ya Baghdad na serikali ya Kikurdi nchini Iraq na kuhakikisha kwamba watu wa asili ya Turkmen wanapata nafasi wanayostahili kwa utulivu wa Iraq.

Rais huyo wa Uturuki pia aliangazia juhudi zinazoendelea za kukomesha ukandamizaji wa Israeli huko Gaza na kusisitiza umuhimu wa mataifa ya Kiislamu kutenda kwa umoja wakati wa mchakato huu.

Kwenye ziara hiyo ya Jumatatu, Erdogan ameambatana na Waziri wa Mambo ya nje wa nchi hiyo Hakan Fidan, Waziri wa Mambo ya ndani Ali Yerlikaya, Waziri wa Ulinzi wa Kitaifa Yasar Guler, Mkurugenzi wa Mawasiliano Fahrettin Altun, mshauri wake Mkuu Akif Cagatay Kilic na mawaziri wengine.

TRT World