Helikopta ya Rais wa Iran Ebrahim Raisi ilianguka katika eneo karibu na mpaka wa Azerbaijan na Iran huku kukiwa na hali mbaya ya hewa na kutoonekana vizuri, kulingana na Tehran na vyombo vyake vya habari rasmi.
Saa chache kabla ya ajali hiyo, Raisi alitembelea Azerbaijan kwa ajili ya kuzindua mradi wa pamoja wa bwawa kwenye mto Aras, kuashiria kuimarika kwa uhusiano kati ya nchi hizo jirani.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Iran, Raisi aliandamana na waziri wake wa mambo ya nje, Hossein Amirabdollahian, na maafisa wengine wakuu.
"Bado hakuna kitu rasmi. Lakini wasiwasi unaongezeka (juu ya hatima ya rais)," anasema Fatima Karimkhan, mwandishi wa habari wa Iran anayeishi Tehran, akizungumzia ajali ya helikopta ya rais katika eneo la milimani katika jimbo la Azerbaijan Mashariki mwa nchi hiyo. Anasema tofauti na ambavyo baadhi ya vyombo vya habari bado vinaripoti, helikopta hiyo haikupata 'kutua kwa shida' bali ajali. "Hakuna dalili ya helikopta. Ni dalili mbaya,” anaiambia TRT World.
Karimkhan hafikirii kuhusika kwa hujuma nyuma ya ajali ya helikopta ya Raisi licha ya ukweli kwamba "baadhi ya vituo visivyo rasmi vilivyounganishwa na Israeli vinatangaza wazo hilo."
Raisi ni nani?
Rais wa Iran mwenye umri wa miaka 64 amejulikana kwa misimamo yake mikali, na aligombea dhidi ya watu wenye msimamo wa wastani na wapenda mageuzi wa Iran kama mgombea wa kihafidhina katika chaguzi zilizopita.
Mnamo mwaka wa 2017, alikuwa mgombea wa chama maarufu cha Front of Islamic Revolution Forces, kambi ya kihafidhina, dhidi ya Hassan Rouhani, rais wa mageuzi wakati huo.
Ingawa alishindwa dhidi ya Rouhani mwaka wa 2017, alishinda uchaguzi wa rais mwaka 2021 baada ya Baraza la Walinzi la nchi hiyo, taasisi inayoamua ni nani kati ya wagombea hao anaweza kugombea, kuwafuta wagombea 32 wa mageuzi na wenye msimamo wa wastani kabla ya uchaguzi.
Wachambuzi wengi waliona uamuzi wa baraza la hadhi ya juu kama kufungua njia ya ushindi wa Raisi. Raisi ambaye hapo awali alishika nyadhifa za juu akiwemo Jaji Mkuu wa Iran, mkuu wa mfumo wa mahakama wa Jamhuri ya Kiislamu, anahesabiwa kuwa mshirika wa Kiongozi Muadhamu Ali Khamenei.
Wachambuzi pia wamemwona kama mrithi anayewezekana wa kiongozi mkuu aliyezeeka. Tangu miaka yake ya mapema, Raisi amepata elimu thabiti ya kidini akiwa mwanafunzi wa seminari ya Qom, chuo kikuu cha kidini cha Iran chenye idadi kubwa ya Shia.
Kukabiliana na vita
Chini ya urais wake, Raisi alikabiliwa na mvutano unaoongezeka kutokana na vita vya Ukraine, ambapo Tehran imeiunga mkono Urusi kimya kimya, kwa kuuza ndege zisizo na rubani za Iran kwa Moscow, kwenye mzozo unaoendelea wa Gaza, ambapo Israel imemshutumu adui wake mkuu kwa kutoa mafunzo kwa wapiganaji wa Hamas na kuwapa silaha.
Raisi pia alisimamia mashambulizi ya Iran ya ndege zisizo na rubani na makombora dhidi ya Israel mwezi uliopita.
Chini ya Raisi, Iran imeendelea kurutubisha madini ya uranium, na hivyo kuongeza ukosoaji wa Magharibi na Israel huku mvutano kati ya Tehran na Washington ukiongezeka.
Marekani ilimuwekea vikwazo Raisi kwa kushiriki kwake katika tume ya mahakama yenye utata ya 1988 kama mwendesha mashtaka. Matokeo yake, alikuwa rais wa kwanza wa Iran kuwekewa vikwazo na Marekani.
Kulingana na ripoti ya Umoja wa Mataifa, alitajwa pia kwa jukumu lake katika mahakama ya Iran, ambayo iliidhinisha kunyongwa kwa angalau watoto tisa kati ya 2018 na 2019.
Serikali ya Raisi pia imekosolewa vikali kwa jinsi ilivyoshughulikia kuwekwa kizuizini kwa kwa Mahsa Amini, kulikozua utata mkubwa hasa kw akuw akulisababisha kifo chake, na kusababisha maandamano makubwa nchini kote mwishoni mwa 2022.
Watraalamu wakidiplomasia wanasema uongozi wake umegubikwa na mchanganyiko wa hisia, ndani na nje ya Iran.