Utamaduni wa Uturuki ya kitaifa, yenye mizizi ya maadili, msimamo wetu wa kihistoria, maadili yetu, uelewa wetu wa siasa" hautoi nafasi ya kukaa kimya au kukataa ukweli kukiwa na tatizo," Fidan alielezea  / Photo: AA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ameikosoa Marekani, na nchi za Magharibi kwa ujumla, kwa uungaji mkono wao usio na masharti kwa Israel katika operesheni zake zisizo na kikomo dhidi ya Gaza ya Palestina.

"Marekani iko katika makubaliano kamili ya kuiunga mkono Israel," Fidan alisema katika mahojiano maalum na TRT Haber siku ya Ijumaa, akisisitiza kuwa ziara ya Rais Joe Biden nchini Israel ni sawa na Marekani kuidhinisha uharibifu mkubwa huko Gaza.

Alisisitiza kuwa wakati Israel inatafuta kulipiza kisasi kwa hasara iliyotokana na mashambulizi ya Hamas mnamo Oktoba 7, "kushindwa kwake kuwatilia maanani raia wakati wa kulipiza kisasi, na kuamua kushambulia watu kwa pamoja inapaswa kuwa chanzo ya kugadhabisha sana.”

Mashambulizi ya Hamas yanatumika kama ushahidi wa sera mbovu za Israel, hasa kwa kushindwa kufanya amani na majirani zake, Fidan alisema, akiongeza kuwa kushindwa kwa Israel kukubali suluhisho la mataifa mawili na Wapalestina ni "kosa la kimkakati tangu mwanzo."

"Shinikizo na ukandamizaji kwa Wapalestina, ambao ni wadau wakuu katika suala hili, limekuwa la kimfumo zaidi, ililoenea, na za mara kwa mara. Ilikuwa dhahiri kwamba hali hii hatimaye ingesababisha mlipuko,” Fidan alieleza.

Vita vya kudumu, ukosefu wa utulivu unatawala eneo hilo

Waziri wa Mambo ya Nje pia aligusia upendeleo katika ukweli uliolazimishwa na nchi za Magharibi, akisisitiza kwamba mtazamo wa Magharibi "unaunga mkono jambo moja nchini Ukraine na jambo lingine huko Palestina."

Aliendelea kueleza kwamba "hakuna uundaji wa sera unaozingatia kanuni za kimaadili za ulimwengu wote," katika nchi za Magharibi, ambapo suala linaloendelea ni "uungaji mkono usio na masharti kwa Israeli katika kila jambo."

Kinyume cha hili, Uturuki imekuwa ikijaribu kuonyesha mtazamo unaoweka kipaumbele usalama na maslahi ya pande zote mbili, Fidan alisisitiza.

"Tunahitaji mazingira ambayo yanatoa nafasi kwa mazungumzo ambayo yatawezesha suluhu ya mataifa mawili ambayo yanatambua haki halali za Wapalestina," Fidan alisema, akisisitiza kuwa Uturuki inafanya kazi kuhakikisha kuwa makubaliano ya amani yanafikiwa.

Waziri wa Mambo ya Nje alionya kwamba ikiwa hatua za haraka hazitachukuliwa kwa ajili ya amani ya kudumu, "vita vya kudumu na ukosefu wa utulivu vitafanyika" katika eneo hilo.

"Kama Uturuki, tunafanya jukumu letu na tutaendelea kufanya hivyo. Katika suala hili, tuna wajibu kwa watu wetu wenyewe na kwa historia, "alisema.

"Utamaduni wa uturuki ya kitaifa, yenye mizizi ya maadili, msimamo wetu wa kihistoria, maadili yetu, uelewa wetu wa siasa" haitoi nafasi ya kukaa kimya au kukataa ukweli kukiwa na shida, aliongeza.

Fidan alisisitiza kwamba Uturuki itaendelea kusimama pamoja na dada na kaka zake wa Kipalestina.

"Nataka wajue kwamba tunafanya kila tuwezalo ... mfumo wetu wote wa misaada, kutoka kwa vyombo vya serikali hadi mashirika yasiyo ya kiserikali, unaweka mbele juhudi za ajabu kuwasilisha misaada kwao," alisema.

TRT Afrika