Katika robo tatu ya mwaka 2023, Uturuki imekuwa nchi ya pili duniani katika kasi ya ukuaji miongoni mwa mataifa ya G20, Erdogan ametangaza. / Picha: AA

Mauzo ya nje ya Uturuki kwa mwaka 2023 yamefikia kiwango cha juu kabisa cha dola bilioni 255.8, ikiongezeka kwa kiwango cha asilimia 0.6 kutoka mwaka jana, Rais Recep Tayyip Erdogan ametangaza.

"Kwa maana hiyo, kiwango kimepita malengo ya mpango wetu wa kati wa dola bilioni 255," Erdogan amesema katika kutangazwa kwa mpango wa mauzo ya nje ujulikanao kama, "2023 Export Figures Announcement Program" siku ya Jumanne.

Uwiano wa mauzo ya nje na uingizaji wa ndani umeongezeka kwa asilimia 0.8 kutoka ile ya mwaka jana ya asilimia 70.7, rais amesema, akisisitiza kwamba biashara ya nje ya nchi imefikia asilimia 3.2 kwa mwaka 2023.

"Isipokuwa kwa mwezi Julai, biashara ilipungua katika kipindi cha miezi saba ya mwaka 2023," alielezea. Akiongeza kwamba, Uturuki inalenga kuimarisha biashara ya nje kwa bidhaa na huduma kwa mwaka 2024 kufikia zaidi ya dola bilioni 375, nchi ina uwezo zaidi wa kufikia lengo hilo," amesema.

Katika robo tatu ya mwaka 2023, Uturuki imeendelea kukuwa bila kizuizi kwa robo 13 kwa kukuwa kwa asilimia 5.9, na kuwa nchi ya mbili kwa ukuaji wa kasi katika mataifa ya G20.

Ukuaji endelevu

Rais Erdogan amesema katika hotuba yake, kwamba licha ya baadhi kutofurahia, Uturuki inaendelea kukuwa, na kuwa na taarifa njema kulingana na kanuni za ukuaji kupitia uwekezaji, ajira, uzalishaji na uuzaji nje.

Amesisitiza umuhimu wa mafanikio katika uchumi, kwa kuzingatia changamoto za miaka ya hivi karibuni, kuanzia ugaidi, majaribio ya kupindua serikali na matukio ya barabarani, na kuvamiwa kwa safaru.

Akionyesha kwamba uchumi wa Uturuki umekuwa kwa kiwango cha asilimia 6 kwa mwaka katika kipindi cha mwaka 2012-2022, ikipita kiwango cha dunia cha asilimia 3.4, Erdogan ametaja kwamba hata changamoto za ulimwengu kama vile janga la Covid-19, mnyororo wa usambazaji umekatizwa, vita kati ya Urusi-Ukraine, na mgogoro wa mali ghafi na mafuta haikupunguza kasi ya ukuaji wa uchumi.

Ametaja ukuaji chanya wa uchumi, kwa ukuaji wa asilimia 14.7 katika uwekezaji katika robo ya tatu ya mwaka 2023, ikionyesha kiwango cha juu katika kipindi cha miaka miwili. Pia amehimiza mchango wa uuzaji nje wa bidhaa na huduma, kwa ukuaji wa bidhaa za ndani, ambao ni asilimia 0.3 katika robo ya tatu ya 2023.

Kupambana na mfumko wa bei kwa kila namna

Akionyesha kuridhishwa na athari za uzalishaji wenye nguvu katika takwimu za hivi karibuni za ajira, Erdogan pia ametaja kwamba zaidi ya ajira milioni 4 za ziada zimetengezwa katika kipindi cha miaka 3 iliyopita ilikinganishwa kabla ya kipindi cha janga.

Erdogan amesisitiza kwamba, kama uchumi wa mataifa mengine duniani, wasiwasi mkubwa wa Uturuki ni mfumko wa bei uliosababishwa na kuongezeka kwa gharama ya maisha, na kusema kwamba wana lenga kupunguza mfumko kwa tarakimu moja bila kuathiri uzalishaji, ajira, na ukuaji wa uchumi.

Hawataruhusu wale wenye tamaa kutumia vibaya nafasi hiyo kuhatarisha maisha ya watu, maendeleo, rasilimali, fedha za watu wa Uturuki, amesema.

Mapambano dhidi ya mfumko wa bei

Kuhusiana na jitihada pacha za kupambana na gharama za maisha, ambapo uthibiti unafanyika upande mmoja, na udhibiti upande mwengine, ameonyesha kurishishwa na jitihada zinazolenga uwekezaji, ajira, na uzalishaji, ikitoa kipaombele cha upatikanaji wa fedha kwa wasafirishaji nje, ambayo mwishowe itaondoa mfumko wa bei kutoka kwa wananchi wa kawaida.

Katika mwaka mgumu wa 2023, uliogubikwa na changamoto na majaribio, Erdogan amethibitisha mapambano yaliyokabili eneo na changamoto za kiuchumi zilizosababishwa na matetemeko ya ardhi ya Februari 6, ambayo yaliongeza mzigo wa dola bilioni 104 kwa uchumi wa Uturuki.

Mbali na kupoteza zaidi ya maisha ya watu 50,000 na uharibifu mkubwa katika majimbo 11, Erdogan amesifu mafanikio ya Uturuki katika kupambana na hali hiyo kwa haraka katika maeneo yote, hasa katika uzalishaji, baada ya "janga la karne," janga la asili ambalo hakuna nchi nyengine ingeweza kukabiliana nalo kwa ufanisi na haraka.

Ametaja athari mbaya ya tetemeko juu ya utumaji bidhaa nje, iilyopungua kwa dola bilioni 6.

Kupambana na siasa za chuki

Akizungumzia chuki dhidi ya Uislamu na kauli dhidi ya waarabu, zilizosababishwa na vyama vya upinzani ndani ya Uturuki, ameshutumu kuenea kwa chuki na kutaja kampeni iliyolenga watalii katika kipindi cha kiangazi, chanzo kikubwa cha fedha kwa nchi.

"Tunakabiliana na hali ambayo inasababisha chuki kwa Uislamu na chuki dhidi ya wageni. Kwa bahati mbaya, wahusika upinzani wana nafasi katika huu uchafu, siasa hatari za chuki."

Ametaja jitihada za Uturuki katika kuongeza marafiki, Erdogan amesema anafahamu majaribio ya kuitikisa nchi kupitia matamko mabaya, hasa wale wanaolenga historia, dini, uchumi, na mahusiano ya kibiashara na nchi ndugu zetu.

"Tunafahamu jitihada za kuitenga nchi yetu na eneo, washiriki wa kikanda, na nchi rafiki ambazo tuna uhusiano wa nguvu, wa kidini, kibinadamu, uchumi, na mafungamano ya kibiashara kupitia maneno ya chuki."

"Uturuki bila shaka itasitisha mchezo huu, kama ilivyosambaratisha mchezo mchafu kabla," amesema.

Erdogan amewataka wafanyabiashara kuwa na jukumu muhimu katika kupambana na siasa za chuki zinazofanywa na mahasimu wa Uturuki. Amewataka wachangie kwa kutoa taarifa sahihi kwa umma, hasa vijana.

Ameonyesha kuridhishwa kwake kwa kuwa na wafanyabiashara waanzilishi ambao, bila kuchoka, kuongeza biashara na kupeleka bidhaa za Uturuki duniani, Erdogan amesema Uturuki iko katika eneo la kimkakati kijiografia.

Erdogan amesisitiza jithada za kuongeza mahusiano na majirani kwa misingi ya "manufaa ya pande zote mbili" na kutatua migogoro na nchi za kikanda kwa kuleta ushirikiano.

Rais pia, amesisitiza jitihada zao kuongeza uhusiano na mataifa ya Turkic kwa kiwango cha juu kihistoria, kukuza mahusiano kwa misingi ya kuheshimiana na bara Ulaya na Marekani, na kukuza mahusiano bora na Afrika, na nchi za Latin America.

TRT World