Ruto alielezea masikitiko yake kuhusu jinsi marais wa Afrika hutendewa vibaya wanaposafiri katika mataifa yaliyoendelea au mikutano na viongozi wa nje wakati wa hotuba yake katika mazungumzo ya Utawala Bora wa Mo Ibrahim katika KICC jijini Nairobi.
"Si jambo la busara kwa marais 54 wa Afrika kwenda kuketi mbele ya bwana mwingine kutoka mahali pengine. Wakati mwingine tunatendewa vibaya, tunapakiwa kwenye mabasi kama watoto wa shule. Si sawa," Ruto alisisitiza.
Kundi la watu sita au saba wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwakilisha Afrika na huo ndio msimamo ninao uchukua kama Rais wa Kenya, kwa mkutano mwingine wowote ambao tutafanya pamoja katika mataifa ya nje.
Alitoa mfano wa mazishi ya marehemu malkia Elizabeth yalivyokuwa kwa marais wa Afrika. Mnamo Septemba 19, 2022, yeye na marais wengine wa nchi za Kiafrika waliletwa na kundi la mabasi hadi mazishi ya Malkia Elizabeth, huku marais wa nchi za Magharibi wakiruhusiwa kwenda huko kwa magari yao binafsi.
Kwa mfano Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden waliruhusiwa kutumia gari lao linalotambulika kama ‘The Beast’ kufika hadi kwenye kanisa.
"Kundi la watu sita au saba wanapaswa kuwa na uwezo wa kuwakilisha Afrika na huo ndio msimamo ninao uchukua kama Rais wa Kenya, kwa mkutano mwingine wowote ambao tutafanya pamoja katika mataifa ya nje." Ruto aliongeza.
Wateule wachache wana uwezo wa kuwakilisha Umoja wa Afrika katika mazungumzo ya kimataifa, kulingana na Rais William Ruto, ambaye alidai kuwa wanachama wa Umoja wa Afrika walifanya uamuzi huo.
"Uamuzi ambao tumefanya kama AU ni kwamba kwenda mbele kama kutakuwa na majadiliano kati ya Afrika na nchi nyingine yoyote tutawakilishwa na mwenyekiti.’ Asema Ruto.
Kulingana na yeye, mataifa ya Afrika yanaheshimu mamlaka ya nchi zingine kwa hivyo isiwe tatizo kwa mataifa ya Kiafrika pia kupewa heshima.