Zaidi ya watu 76 wanakabiliwa na mashtaka ya uhaini na jaribio la mapinduzi kufuatia maandamano mwezo Agosti kulalamikia uchumi mgumu / Picha: Reuters 

Rais wa Nigeria Bola Tinubu aliagiza kwamba watoto wote waliozuiliwa wakati wa maandamano dhidi ya serikali mwezi Agosti waachiliwe huru na mashtaka ya uhaini dhidi yao yafutwe, Waziri wa Habari Mohammed Idris alisema Jumatatu.

Takriban watu 76, wakiwemo watoto 30, walishtakiwa kwa uhaini na kuchochea mapinduzi kwa kushiriki katika maandamano mabaya ya Agosti dhidi ya matatizo ya kiuchumi.

Amnesty International ilisema takriban watu 22 walikufa wakati wa maandamano katika mapigano na vikosi vya usalama.

Kufikishwa mahakamani kwa watoto hao kulizua hasira ya umma na ukosoaji wa serikali Ijumaa iliyopita.

“Rais ameagiza watoto hawa.... hawa wadogo waachiwe mara moja,” Idris alisema. Watoto hao walipewa dhamana siku ya Ijumaa na kesi yao ilipangwa kuanza Januari.

Mwezi Agosti, maelfu ya Wanigeria waliandamana katika mji mkuu wa kibiashara wa Lagos, Abuja, na miji mingine kadhaa kupinga mageuzi ya kiuchumi ya Tinubu ambayo yamechochea mfumuko wa bei na kusababisha mgogoro mbaya zaidi wa gharama za maisha katika kizazi.

Rais Tinubu ameapa kufuatilia mabadiliko ambayo anasema yanahitajika ili kuiweka nchi sawa.

Reuters