Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema akizungumza na wananchi wa Nyamongo, Tarime vijijini.
Baadae hii leo kiongozi huyo atazindua kampeni kanda ya Serengeti. Kwa mujibu wa Chadema, uzinduzi huo utafanyika katika jimbo la Tarime mjini.
Kampeni hizi za vyama vya kisiasa nchini Tanzania ni kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika November 27 mwaka huu.
Hata hivyo, kumekuwa na malalamiko kutoka baadhi ya vyama vya upinzani nchini humo wakidai kuenguliwa kwa baadhi ya viongozi wao.
Kwa upande wake, Waziri wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa, amesema kwamba baadhi ya wagombea wa vyama mbalimbali ambao awali waliwasilisha malalamiko yao kwa mamlaka zinazohusika na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa nchini humo tayari wamerejeshwa katika nafasi zao.