| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Mbunge wa Marekani aanza mchakato wa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Waziri wa Ulinzi
Mbunge wa chama cha Democrat Yassamin Ansari ameshtumu uongozi wa wizara ya ulinzi kwa kuchochea vita zaidi na kusababisha vifo vya raia na hofu ya kisheria.
Mbunge wa Marekani aanza mchakato wa kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Waziri wa Ulinzi
Mbunge wa Marekani Yassamin Ansari anasema Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth “anahusika” katika uhalifu wa kivita. / AP
tokea masaa 9

Mjumbe wa bunge la wawakilishi la Marekani Yassamin Ansari alisema siku ya Jumatatu atawasilisha vifungu vya kura ya kutokuwa na imani dhidi ya Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth, akismhtumu kwa kuchochea “vita visivyo halali” dhidi ya Iran.

Ansari, mwanachama wa chama cha Democrat kutoka Arizona, anasema Rais Donald Trump anachochea mapigano hayo kwa kushambulia miundombinu ya raia, akiongeza kuwa Hegseth “anashiriki uchochezi” katika hatua ambazo ameonya zinaweza kuwa za vita vya uhalifu.

“Nimetaka utekelezwaji wa sheria ya kutokuwa na imani na rais itumike na pia nawasilisha vifungu vingine vya kura ya kutokuwa na imani,” alisema katika taarifa kwenye mitandao ya kijamii.

Kuongezeka kwa tathmini kutokana na mauaji ya raia

Hatua hii inakuja huku shinikizo zikiongezeka kuhusu vita vya jeshi la Marekani nchini Iran. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa kombora la Marekani lilishambulia shulr moja ya msingi mwezi Februari, na kuwaua watu wasiopungua 175 — wengi wao wakiwa watoto.

Trump pia anashutumiwa kwa kutishia kushambulia miundombinu kama mitambo ya kufua umeme na madaraja, huku wataalamu wa sheria wakionya kuwa hatua hizo zinaweza kukiuka sheria ya kimataifa.

Vita vimeendelea kote katika kanda

Hali ya taharuki imetanda tangu Marekani na Israel ilipoanzisha vita vya pamoja dhidi ya Iran Februari 28, huku mamlaka za Iran zikiripoti kuwa watu zaidi 1,300 wameuawa, ikiwemo viongozi waandamizi.

Iran imejibu kwa kurusha makombora na mashambulizi ya ndege zisizo na rubani ikilenga Israel, maeneo yanayohusiana na Marekani, na mataifa ya Ghuba yaliyo na kambi za kijeshi za Marekani na taasisi za kifedha kote katika kanda, wakati wakizuia meli kupita Mlango Bahari wa Hormuz — hatua ambayo imetatiza masoko ya nishati kote duniani.

CHANZO:AA