| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Waziri wa ulinzi wa Mali ameuawa katika shambulio la kigaidi: Al Jazeera
Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara ameuawa katika shambulio la kigaidi akiwa nyumbani kwake siku ya Jumamosi, Al Jazeera ilikuwa ya kwanza kutoa taarifa hiyo siku ya Jumapili.
Waziri wa ulinzi wa Mali ameuawa katika shambulio la kigaidi: Al Jazeera
Sadio Camara, waziri wa ulinzi wa Mali, ameripotiwa kuuawa katika mashambulizi Aprili 25, 2026. / Wengine

Waziri wa Ulinzi wa Mali Sadio Camara ameuawa katika shambulio la kigaidi akiwa nyumbani kwake siku ya Jumamosi, Al Jazeera ilikuwa ya kwanza kutoa taarifa hiyo siku ya Jumapili. Ikitaja vyanzo vya familia, AFP pia ikathibitisha kifo cha waziri huyo.

Nyumba ya Camara katika eneo la Kati, mji ulioko kilomita 15 kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa Mali Bamako, ilishambuliwa kwa mabomu, ambayo yaliharibu nyumba hiyo, AFP imeripoti.

Camara alipelekwa hospitali mjini Bamako, lakini akafariki dunia, kulingana na Al Jazeera, ambayo imenukuu vyanzo vya uhakika.

Siku ya Jumapili asubuhi, idadi kubwa ya wanajeshi ilikuwa nje ya hospitali ambayo Camara alikuwa anatibiwa, AFP iliripoti. Mapema wasaidizi wake walikanusha taarifa kuwa mashambulizi ya kigaidi yalikuwa yamemjeruhi.

Mtu muhimu kwenye serikali

Serikali ya Mali bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ya Camara.

Kifo cha Sadio Camara ni cha afisa wa ngazi za juu wa serikali kilichotokana na mashambulizi haya ya kigaidi nchini Mali, ambayo, hadi hivi karibuni, yalikuwa yanalenga raia na wanajeshi.

Camara alikuwa mtu muhimu katika serikali ya Mali, na alikuwa na uhusiano mzuri na Rais wa nchi, Assimi Goita.

Camara amekuwa waziri wa ulinzi wa Mali katika vipindi viwili tofauti — mara ya kwanza kati ya Oktoba 2020 na Mei 2021, na tena, kuanzia Juni 2021 hadi kile kinachoaminika kuwa kifo chake Aprili 26, 2026.

Mashambulizi

Mwanajeshi huyo wa ngazi za juu aliyepata mafunzo yake nchini Mali na Urusi amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 47.

Mali imeshambuliwa na magaidi siku ya Jumamosi, huku miji kadhaa, ikiwemo mji mkuu, ikilengwa na magaidi na wanaotaka kujitenga.

Watu wasiopungua 16 waliuawa na mashambulizi hayo, kulingana na serikali. Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Uturuki wameshtumu mashambulizi hayo.

Siku ya Jumapili, hali ilikuwa shwari kidogo, ingawa mapigano mengine yaliripotiwa katika mji wa kaskazini wa Kidal. Jeshi linakabiliana na Tuareg wanaotaka kujitenga.

CHANZO:TRT Afrika and agencies