“Walikuja kwetu wakasema wako tayari kufungua mlango huo. Watu wangu wote walifurahi, isipokuwa mimi,” Rais Trump alisema.
“Nilisema, tukifungua, watapata dola milioni 500 kwa siku. Sitaki hilo litokee hadi suala hili litakapotatuliwa. Hivyo mimi ndiye niliyeufunga.”
Kuhusu bei ya mafuta, Trump alisema Wamarekani wanapaswa kutarajia ongezeko la bei “kwa muda mfupi,” akihusisha hali hiyo na athari za vita vinavyoendelea.
Kwa ujumla, vita vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vimesababisha kupanda kwa bei za nishati duniani.
Trump alisisitiza kuwa lengo lake ni kuhakikisha Iran haina silaha za nyuklia ambazo zinaweza “kulenga kulipua miji ya Marekani au kuleta maafa makubwa katika Mashariki ya Kati.”
Iran imekanusha madai ya kutaka kutengeneza silaha za nyuklia, nayo Shirika la Umoja wa Mataifa la kudhibit masuala ya nyuklia limesema kabla ya vita, hakukuwa na dalili kwamba bomu la atomiki lilikuwa karibu kutengenezwa.
Kwa historia, Marekani ndiyo nchi pekee iliyowahi kutumia silaha za nyuklia vitani, kwa kushambulia miji ya Hiroshima na Nagasaki nchini Japan mwishoni mwa Vita vya Pili vya Dunia, mashambulizi yaliyoua takribani watu 214,000.
Mshirika wa Marekani, Israel, anaaminika kwa muda mrefu kuwa na silaha za nyuklia, ingawa hajawahi kukiri rasmi hadharani.














