| Swahili
ULIMWENGU
5 dk kusoma
Iran haitofungua tena Mlango Bahari wa Hormuz iwapo jeshi la wanamaji la Marekani litaendelea kuwepo
Iran imezuia meli mbili na kusisitiza kuwa kusitishwa mapigano hakuna maana kama vikosi vya Marekani vitaendelea kuzuia meli kupita, huku bei za mafuta zikipanda.
Iran haitofungua tena Mlango Bahari wa Hormuz iwapo jeshi la wanamaji la Marekani litaendelea kuwepo
Meli yenye bendera ya Jordan "Baghdad" ikiwa Ghuba kuelekea Mlango Bahari wa Hormuz, UAE, Jumatano, Aprili 22 2026. / AP

Iran imeapa kutofungua Mlango Bahari wa Hormuz, iwapo jeshi la wanamaji la Marekani litaendelea kuwepo huko, huku taifa hilo la Ghuba likizuia meli mbili zilizokuwa zikijaribu kuvuka njia hiyo ya kimkakati ya bahari.

Idara ya Jeshi la Marekani ya CENTCOM ilisema Jumatano jioni kuwa pia "imeziagiza meli 31 kurudi bandarini" ikiwa ni sehemu ya njia "vizuizi kwa Iran".

Huku kukiwa na hofu ya kuanza tena vita ambavyo vimekumba kanda hiyo, Rais wa Marekani Donald Trump amesema Jumanne kuwa ataendeleza makubaliano ili kuruhusu muda zaidi kwa mazungumzo ya amani yanayoratibiwa na Pakistan.

Iran inasema imeridhishwa na juhudi za Pakistan lakini haikuzungumzia kuhusu kauli ya Trump.

"Kusitishwa mapigano kikamilifu ndiyo kutaleta maana kama hakutakiukwa kwa vizuizi vya jeshi la wanamaji," amesema spika wa bunge la Iran Mohammad Bagher Ghalibaf, ambaye aliongozi ujumbe wa Iran katika hatua ya kwanza ya mazungumzo mjini Islamabad.

"Kufungua Mlango Bahari wa Hormuz haiwezekani huku kukiwa na ukiukwaji wa wazi wa usitishaji mapigano."

Bei za mafuta zilipanda kwa asilimia nne kabla ya kupatika kwa afuweni siku ya Alhamisi baada ya Iran kuapa kutofungua tena Mlango Bahari wa Hormuz iwapo jeshi la wanamaji la Marekani litaendelea kuwepo.

Trump anasema anataka kuupa uongozi wa Iran "unaoweweseka" muda wa kuandaa mapendekezo, katika hatua inayoonekana na wachanganuzi wengi kama kuepuka kuanza tena kwa vita.

Trump aliliambia gazeti la New York Post kuwa mazungumzo huenda yakaanza tena nchini Pakistan katika siku mbili au tatu zijazo, ingawa Iran haijathibitisha kuhudhuria kwake na Makamu wa Rais JD Vance aliahirisha safari yake ya kwenda Islamabad siku ya Jumanne.

Trump pia amesema pia kwa ombi lake Iran imesisitisha kuwanyonga wanawake wanne waliokamatwa wakati wa maandamano ya kupinga serikali wiki kadhaa kabla ya mashambulizi kuanza.

Lakini mahakama nchini Iran zilieleza matamshi yake kuwa "taarifa za kupotosha", akisema wanawake hawajawahi kukabiliwa na hukumu ya kunyongwa nchini humo.

Meli kuzuia

Jeshi la Mapinduzi la Iran linasema limeelekeza meli mbili kwenye fukwe zake kutoka Mlango Bahari wa Hormuz, njia inayotumika kupitisha humusi ya mafuta ya dunia.

"Jeshi la wanamaji la Mapinduzi la Iran asubuhi hii limezuia meli mbili ambazo zimekiuka utaratibu wa Mlango Bahari wa Hormuz," jeshi hilo lilisema katika taarifa.

Lilitaja meli hizo kama ya kontena yenye bendera ya Panama MSC Francesca na nyingine yenye bendera ya Liberia, Epaminondas.

Wizara ya mambo ya nje ya Panama imethibitisha kuzuia kwa meli ya MSC Francesca, ikisema kuwa ni "shambulizi hatari kwa usalama wa baharini" na "uhasama usio wa lazima".

Shirika la linalofuatilia usalama baharini lenye makao yake nchini Uingereza limethibitisha kuwa meli tatu zimeripoti matukio yaliyohusisha ufyatulianaji wa rissi katika Mlango Bahari huo.

Miongoni mwao, meli ya kontena kufyatuliwa risasi na Jeshi la Mapinduzi kaskazini mashariki kwa Oman, kuisababishia uharibifu ingawa hakuna yeyote aliyejeruhiwa, monitor UKMTO imesema.

Chini ya maagizo ya Trump, Jeshi la Wanamaji la Marekani linajaribu kuzuia meli zinazotoka au kuelekea bandari za Iran, ikitaka kuweka shinikizo kwa uchumi wa Iran hata wakati hakuna vita.

Huku kukiwa na vizuizi, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imetangaza Jumatano kuwa Katibu wa Masuala ya Jeshi la Wanamaji John Phelan ataachia ngazi "mara moja".

Haikutaja sababu ya kuondoka kwake ghafla, ikiwa ni afisa mwingine mwandamizi kuondolewa chini ya Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth.

Kaltika kulipa kisasi kwa kushambuliwa Iran imesema kuwa meli lazima ziombe ruhusa zikitaka kuondoka au kuingia Ghuba kupitia Mlango Bahari huo. Awali ilikuwa imeahidi hakuna meli itakayozuiwa wakati wa usitishaji wa mapigano lakini ikabadilisha msimamo wake kutokana na zuio la Trump.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilisema siku ya Jumanne kuwa vikosi vyake vimefanikiwa kuzuia na kuingia ndani ya meli ambayo "haijulikani taifa lake na imewekewa vikwazo". AFP imetambua meli hiyo kuwa moja iliyokuwa inahusishwa na shughuli za Iran. Pande zote mbili zinalaumiana kwa kukiuka usitishaji mapigano.

Mashambulizi zaidi Lebanon kabla mazungumzo

Baada ya kusitisha mapigano na Iran, Marekani imesaidia kupatikana kwa makubaliano ya amani kati ya Israel na Lebanon.

Licha ya makubaliano kutangazwa, mashambulizi ya Israel yamewaua watu watano zaidi siku ya Jumatano, vyombo vya habari vya Lebanon vimesema.

Amal Khalil, mwandishi wa habari wa gazeti la Al-Akhbar, aliuawa na mwandishi mwenzake Zeinab Faraj kujeruhiwa katika shambulio la Israel karibu na mpakani, gazeti hilo lilisema.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza kuwa mwanajeshi wa pili wa Ufaransa, ambaye alijeruhiwa mwishoni wa wiki kutokana na mashambulizi dhidi walinda amani wa Umoja wa Mataifa Lebanon akilaumu kundi la Hezbollah, amefariki dunia.

Mwanajeshi wa kwanza alipigwa risasi na kuuawa katika mashambulizi ya Jumamosi, ambapo Hezbollah wamekanusha kuhusika.

Israel na Lebanon, ambapo mataifa hayo mawili hayana uhusiano wa kidiplomasia, watafanya raundi ya pili ya mazungumzo jijini Washington siku ya Alhamisi.

Lebanon itaomba kuongezwa kwa mwezi mmoja wa kusitisha mapigano wakati wa mkutano huo, afisa mmoja wa Lebanon ameiambia AFP.

Lebanon pia itataka "kusitishwa kwa mashambulizi ya Israel na uharibifu katika maeneo ambayo wako na hakikisho la usitishaji mapigano", afisa huyo amesema, akizungumza kwa masharti ya kutotambuliwa kutokana na umuhimu wa mazungumzo hayo.

Mashambulizi ya Israel kwa Lebanon yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 2,450 tamgu kuanza kwa vita, kulingana na mamlaka za Lebanon.

CHANZO:TRT Afrika Swahili