| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Tamasha kubwa la sayansi kwa vijana barani Afrika limefanyika Côte d'Ivoire
Tamasha la Sayansi Afrika 2026: Tamasha kubwa la sayansi kwa vijana barani Afrika limefanyika mjini Abidjan, Côte d'Ivoire, likiwa na washiriki kutoka nchi takriban 27 za Afrika.
Tamasha kubwa la sayansi kwa vijana barani Afrika limefanyika Côte d'Ivoire
Tamasha hilo lilihudhuriwa na wageni muhimu, akiwemo Deniz Erdoğan Barım, Balozi wa Uturuki Cote d'Ivoire. / / TRT Afrika

Tumasha hilo la kila mwaka, limeandaliwa na Taasisi ya Uturuki ya Maarif, ni jukwaa muhimu la kimataifa lenye lengo la kuboresha ushirikiano katika sayansi, teknolojia na elimu.

Linajumuisha mashindano ya sayansi, ubunifu wa wanasayansi chipukizi pamoja na majadiliano.

Aprili 21, tamasha hilo lilihudhuriwa na wageni muhimu, akiwemo Deniz Erdoğan Barım, Balozi wa Uturuki Cote d'Ivoire.

"Kuwekeza kwa vijana ni uwekezaji katika amani na maendeleo. Ni uwekezaji katika mustakbali endelevu," amesema rais wa Taasisi ya Maarif Mahmut Özdil katika hutuba yake ya ufunguzi.

Tuzo zilitolewa kwa vikundi bora kutoka nchi mbalimbali, ikiwemo Guinea, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Somalia, Gabon, Cameroon, Tanzania, Ghana, Mali, Chad, Tunisia, Burundi, na nchi mwenyeji Côte d'Ivoire.