Jeshi la Israel limethibitisha kuwa mmoja wa wanajeshi wake, alihusika katika kuharibu sanamu ya Yesu kusini mwa Lebanon.
Israel imekiri kutokea kwa tukio hilo, kufuatia hasira kali iliyoibuka baada ya picha mjongeo kumuonesha askari huyo akiharibu sanamu ya Yesu kwa kutumia nyundo kubwa katika mji wa Deir Siryan.
Kulingana na jeshi hilo, askari huyo alikuwa akifanya kazi zake kusini mwa Lebanon.
Kukiri kwa Israel kunakuja wakati ambapo nchi hiyo imeweka wazi kuwa, haina nia yoyote ya kuharibu miundombinu na majengo ya ibada.
Licha ya kukiri kutokea kwa tukio hilo, Israel haikuwa tayari kuweka hazi hatua zitakazochukuliwa dhidi ya mwanajeshi huyo, wala kuweka hadharani utambulisho wake.
Mbunge wa zamani wa Marekani, Marjorie Taylor Greene alionesha kukasirishwa na taarifa hizo, akihoji ushirika wa Marekani na Israel.
Vyombo vya habari vya Lebanon, vimeripoti kuhusu uharibifu mwingine katika eneo la Kikristo katika kijiji cha Ain Ebel.

















