| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Ripoti ya Jaji Chande yakiri kuwepo kwa vifo katika vurugu za baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kupitia chanzo rasmi kutoa idadi ya watu waliopoteza maisha wakati wa vurugu hizo.
Ripoti ya Jaji Chande yakiri kuwepo kwa vifo katika vurugu za baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba
Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman. Picha/ Ikulu Tanzania. / TRT Afrika Swahili

Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani wakati na baada ya Uchaguzi  Mkuu wa Oktoba, 2025, imekiri kwamba vifo vilivyotokea wakati huo vimeacha pengo kubwa kwa familia hivyo kusababisha athari za kiuchumi na utegemezi katika jamii.

Ripoti hiyo imewasilishwa hii leo na Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman kwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ikulu jijini Dar es Salaam.

"Idadi ya vifo 518 inaweza kuwa sio ya mwisho kwani baadhi ya watu au ndugu zao waliamua kwenda kutibiwa maeneo binafsi," amesema Jaji Mkuu Mstaafu.

Hii ni mara ya kwanza kwa serikali kupitia chanzo rasmi kutoa idadi ya watu waliopoteza maisha wakati wa vurugu hizo.  Hata hivyo, takwimu hizi, zimetiliwa mashaka, kufuatia madai ya kuwepo kwa idadi kubwa ya watu wanaodaiwa kufariki.

Matokeo ya Tume hii yamekuwa yakisubiriwa kwa hamu tangu kuundwa kwake na Rais wa Tanzania Novemba 18, 2025.

Tume hiyo ilikuwa ilipewa muda wa siku 90 kukamilisha ripoti yake, hata hivyo, baadae iliongezewa muda wa uwasilishaji hadi Aprili 27, badala ya ile ya awali ya Aprili 3, 2026.