| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Matamshi ya Rais Ruto kuhusu Kiingereza kinachozungumzwa na Wanigeria chazua gumzo mtandaoni
Rais William Ruto wa Kenya, amezua gumzo mitandaoni baada ya kudai kuwa utahitaji mkalimani kumuelewa mzungumzaji wa lugha ya Kiingereza mwenye lafudhi ya Kinigeria.
Matamshi ya Rais Ruto kuhusu Kiingereza kinachozungumzwa na Wanigeria chazua gumzo mtandaoni
Rais Ruto wa Kenya amesema kuwa mfumo wa elimu wa nchi hiyo huzalisha ufasaha mzuri wa Kiingereza. / Reuters

Akizungumza na Wakenya waishio nchini Italia, Rais Ruto alijinasibu kuwa, Wakenya wanazungumza Kiingereza ‘fasaha’ zaidi duniani.

Ruto alisema: “Ukimsikiliza Mnigeria akiongea, huwezi kujua anachosema — unahitaji mkalimani,” huku akijigamba kuwa Wakenya huzungumza “Kiingereza fasaha zaidi duniani.”

Kauli yake, iliibua gumzo na mjadala mkubwa kutoka kwa Wanaigeria na raia wengine mitandaoni, wengi wakimshutumu kiongozi huyo kwa kuidhalilisha nchi nyingine ya Kiafrika.

Kama makoloni ya zamani ya Uingereza, Kenya na Nigeria zote zinatumia Kiingereza kama lugha rasmi, lakini kila nchi imeendeleza mitindo yake tofauti ya matamshi yenye miundo tofauti ya sauti.

Hata hivyo, katika hotuba yake aliongeza kuwa mfumo wa elimu wa Kenya huzalisha ufasaha mzuri wa Kiingereza.

CHANZO:TRT Afrika