| Swahili
ULIMWENGU
2 dk kusoma
Trump asema tukio la risasi 'halitomzuia' kushinda vita vya Iran
Trump anasema tukio la kufyatulia risasi wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa ajili ya waandishi wa habari wa Ikulu ya White House halitaathiri malengo yake ya vita vya Iran huku mshukiwa akitarajiwa kufikishwa mahakamani.
Trump asema tukio la risasi 'halitomzuia' kushinda vita vya Iran
Trump anasema tukio hilo la risasi 'halitomzuia' kushinda vita vya Iran / Reuters

Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku ya Jumamosi kuwa tukio la risasi wakati wa hafla ya chakula cha jioni halitomzuia kushinda vita vya Iran, ingawa anaamini tukio hilo haliwezi kuhusishwa na mzozo huo.

"Hili halitanizuia mimi kushinda vita vya Iran. Sidhani kama hilo lilikuwa na uhusiano wowote na vita, kwa kweli sidhani, kwa kile ambacho tunafahamu," Trump aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano Ikulu baada ya tukio hilo la kushtusha kiusalama.

Hata hivyo awali Trump alikuwa amesema, kuwa "huwezi kujua" linaweza kuhusishwa na vita vya Iran, na kusema wachunguzi wanaendelea kufahamu lengo na mtu huyo aliyefyatua risasi, ambaye wanamueleza kuwa "alikuwa peke yake."

Mshukiwa huyo anayeshtumiwa kwa kuvamia hafla hiyo ya waandishi wa habari iliokuwa imehudhuriwa na Rais Donald Trump atafikishwa mahakamani siku ya Jumatatu, mwendesha mashtaka amesema.

Mshukiwa huyo, ambaye aliyefyatuliana risasi na maafisa wa ulinzi wa viongozi hakupigwa risasi, atafikishwa mahakamani Jumatatu.

Kulingana na Mwanasheria wa Marekani Jeanine Piro, mshukiwa huyo atashtakiwa kwa kutumia silaha katika uhalifu wa vurugu na kumshambulia afisa wa serikali kwa kutumia silaha hatari.

Mapema siku ya Jumamosi kiongozi huyo wa Marekani alifuta safari ya wajumbe wake kuelekea Pakistan kwa ajili ya mazungumzo ya amani na Iran, baada ya kutoridhishwa na msimamo wa Iran katika majadiliano kufuatia vita vya karibu miezi miwili.

CHANZO:TRT Afrika Swahili