| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Jeshi la Mali lasema hali iko shwari sasa baada ya mashambulizi ya kigaidi
Jeshi linasema magaidi kadhaa wamekatwa makali na silaha zao kuharibiwa.
Jeshi la Mali lasema hali iko shwari sasa baada ya mashambulizi ya kigaidi
PICHA YA MAKTABA: Mwanajeshi wa Mali wakati wa kufanya mazoezi. / Reuters

Siku ya Jumamosi jeshi la Mali limesema kuwa hali kote nchini "iko shwari" baada ya kile walichokiita "makundi ya kigaidi" ambayo awali yalikuwa yamefanya mashambulizi asubuhi katika mji mkuu, Bamako, na maeneo mengine ya nchi.

Katika taarifa, jeshi limesema washambuliaji "walizidiwa", licha ya ufyatulianaji wa risasi kusikika na helikopta kuwepo katika anga ya Bamako.

"Makundi ya kigaidi, ambayo bado hayajatambulika, mapema asubuhi yalilshambulia maeneo kadhaa na kambi ya jeshi katika mji mkuu na sehemu za vijijini" za nchi.”

"Tunatoa wito kwa raia kuwa makini. Vikosi vyetu vya ulinzi na usalama vinakabiliana na hao washambuliaji," taarifa iliongeza.

Kulikuwa na mapigano maeneo ya mji wa Bamako, sehemu za Gao na Kidal kaskazini mwa nchi, na katika mji wa kati wa Sevare.

Ufyatulianaji wa risasi ulisikika eneo la Kati, katika mitaa ya Bamako.

Taarifa ya jeshi iliongeza kuwa "magaidi kadhaa walikatwa makali na silaha zao kuharibiwa".

Chanzo cha polisi kimeiambia Anadolu kuwa uwanja wa ndege umedhibitiwa, huku maafisa wakishika doria katika maeneo ya karibu.

Mali imekuwa katika hali ya ukosefu wa usalama tangu 2012, huku makundi yenye silaha yakishambulia maeneo ya kijeshi na kiraia kote nchini.

Kiongozi wa sasa wa nchi hiyo ni Jenerali Assimi Goita, ambaye ni rais wa mpito. Amekuwa madarakani tangu mapinduzi ya pili ya kijeshi Mei 2021, alipompindua rais aliyekuwepo na kuchukua uongozi wa serikali ya mpito. 

CHANZO:TRT Afrika and agencies