Maelfu ya maandishi yanayoaminika kuandikwa katika karne ya 14 yamegundulika katika nyumba za zamani za watawa zilizoko karibu na Mlima Athos nchini Ugiriki.
Mtafiti na msomi Jannis Niehoff-Panagiotidis anasema kuwa: “Maandishi haya zaidi ya 25,000 yaliandikwa kati ya mwaka 1371 na 1374 na yanaeleza ukweli kuhusu kilichojiri wakati Waotomani waliwasili Ugiriki ya kaskazini.”
Kwa mujibu wa Jannis, historia hiyo ni ya kale kuliko hata ile ya Instanbul sehemu ambayo Waotomani waliupa jina Constantinnople mji mkuu huo. Inasadikiwa hilo lilitendeka katika karne ya 15 hivyo basi kufanya maandishi yaliyopatikana Mlima Athos kuwa ya zamani zaidi.
Zannis anaongeza kuwa ni vigumu kuilewa vizuri jamii na uchumi wa Mlima Athos bila ya kuzingatia maandishi hayo.
Taswira mpya kuhusu utawala wa Waotomani
Maktaba ya watawa ya Pantokrator inasadikiwa kujengwa zaidi ya miaka 1000 iliyopita ina maandishi mengi kwa lugha tofauti ikiwemo Kigiriki, Kirusi na Kiromania. Mengi ya maandishi hayo yamesomwa isipokuwa yale Kiotomani kwa lugha ya Turkiye.
Maandishi hayo yanaeleza ukweli kuhusu kilichoendelea Mlima Athos ambapo Waotomani waliutunza na kuulinda dhidi ya uvamizi kutoka nje.
Niehoff-Panagiotidis anasema kuwa moja kati ya hatua alizochukua Kiongozi wa Waotomani Murad II, alipofanikiwa kuuteka Mji wa Thessaloniki – mji katibu zaidi na Mlima Athos---ilikuwa ni kutunga sheria madhubuti za kuilinda jamii ya eneo hilo mwaka 1430.
“Hilo linaonesha hali hali halisi. Sultani mwenyewe alihakikisha kuwa Mlima Athos unalindwa na kutunzwa ipasavyo.” Anasema Niehoff-Panagiotidis.
Aidha anaongeza kuwa hata kabla ya hilo kufanyika, tayari Sultan alikuwa ameagiza adhabu kali kwa yeyote mgeni atakayejaribu kuvamia Athos. Agizo hilo lilitokana na kitendo cha wizi kilichotekelezwa na wavamiza mlimani hapo.
“Jeshi la Sultan hata lenyewe halikukita kambi mlima Athos. Walikuwa tu na mwakilishi mkazi wa Athos ambaye alibaki tu kwenye kituo akinywa chai labda.”
Jambo linguine lililogundulika kwenye maandishi hayo kwa mujibu wa Niehoff-Panagiotidis ni kuwa utawala wa Waotomani haukulazimisha yeyote kufuata sheria ya Kiislamu katika Mlima Athos na Ugiriki ya Kaskazini kwa ujumla.
Aidha Padre Theophilos wa Pantakrator, ambaye anasidia kung’amua ukweli ulioko kwenye maandishi hayo anasema: “Utafiti huo unafichua jinsi gani binadamu wanaweza kuishi pamoja kwa kuheshimiana na kuheshimu haki za kila mmoja.”