Vijana wanakabiliwa na wimbi ya machafuko ambayo hayajawahi kutokea, na unyanyasaji wa kingono unaosababishwa na vita, mabadiliko ya tabia nchi, njaa, na ukosefu wa makazi, ametahadharisha Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia unyanyasaji dhidi ya watoto.
"Watoto hawahusiki na vita. Hawahusiki na matatizo ya hali ya hewa. Na wanapata taabu sana," amesema Najat Maalla M'jid, Mjumbe Maalaumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulika na unyanyasaji dhidi ya watoto.
"Vurugu dhidi ya watoto zimeongezeka kwa kiwango kikubwa, zimesababishwa na migogoro inayohusiana," amesema.
M'jid, ambae ni daktari wa watoto kutoka Morocco, Alhamisi atawasilisha ripoti kwa Umoja wa Mataifa inayoonyesha ukatili unaofanywa dhidi ya watoto, na kwamba teknolojia inachangia kuongeza uhalifu dhidi ya vijana tofauti na ilivyokuwa mwanzo.
"Kusitisha machafuko inawezekana, na pia inatija za kiuchumi," M'jid ameiambia AFP, na kusisitiza kwamba watu wengi duniani wana azma ya kumaliza tatizo hilo.
"Tatizo ni jinsi ya kuwaunga mkono, na kutumia njia zote."
Lakini suluhu inahitajika sana, ripoti yake inaonyesha.
Zaidi ya watoto milioni 450 wameishi katika maeneo yenye migogoro mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka 2022, asilimia 40 ya watu milioni 120 waliokosa makazi mwishoni mwa Aprili walikuwa watoto, na milioni 333 ya watoto wanaishi katika ufukara.
Hii inachangiwa na zaidi ya watoto bilioni 1 walio katika hatari ya kuathirika na mabadiliko ya tabia nchi, ambayo yana athari nyingi.
'Wazazi wa baadae'
Ndoa za utotoni ni janga lililoenea, M'jid ametahadharisha, huku kukiwa na zaidi waathirika 640.
Zaidi ya wanawake na wasichana milioni 370 walikabiliwa na ubakaji au unyanyasaji wa kijinsia wakati wa utoto wao, kwa mujibu wa taarifa nyengine ya UNICEF.
"Watoto wanaweza kuwa waathirika wa unyanyasaji, mitandaoni au nje ya mitandao. Wanaweza kuwa waathirika wa ajira za utotoni, utumwa, na vitu vingi, na hata watoto wenye silaha katika migogoro," M'jid amesema.
Ametahadharisha kwamba, kukosekana kwa usalama kunakosababishwa na mapigano katika jamii mbalimbali duniani, kama Sudan na Haiti, mapigano yanakuwa jambo la kawaida."
"Watoto wako wanapokabiliana na unyanyasaji wakiwa wadogo, wakiona hivyo tu, unawezaji kukabiliana na hali hiyo?"