Rais Vladimir Putin alisema kuwa Urusi inatarajia kurekodi mavuno ya juu mwaka huu. / Picha: Reuters 

Urusi itachukua nafasi ya mauzo ya nafaka ya Ukraine barani Afrika, Rais Vladimir Putin amesema, baada ya Moscow kujiondoa katika makubaliano ya kuruhusu usafirishaji wao salama.

"Urusi itaendelea na juhudi zake za kutoa usambazaji wa nafaka, bidhaa za chakula, mbolea na bidhaa nyingine kwa Afrika," Putin alisema katika taarifa iliyochapishwa Jumatatu kwenye tovuti ya Kremlin.

"Nataka kutoa hakikisho kwamba nchi yetu ina uwezo wa kuchukua nafasi ya nafaka ya Ukreni kwa misingi ya kibiashara na bila malipo."

Operesheni ya kijeshi ya Moscow iliziba bandari za Bahari Nyeusi za Ukraine kwa meli za kivita hadi makubaliano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa na Uturuki na kutiwa saini Julai 2022 kuruhusiwa kupitisha usafirishaji wa nafaka muhimu uheshimiwe.

Mapema mwezi Julai Urusi ilijiondoa katika makubaliano hayo baada ya kulalamika kwamba makubaliano kuhusiana na kuruhusu uuzaji nje wa chakula na mbolea ya Urusi hayajazingatiwa.

Moscow baadaye ilisema itazingatia meli za mizigo zinazosafiri kwenda Ukraine kupitia Bahari Nyeusi kuwa meli za kijeshi.

Malalamiko ya Afrika

Umoja wa Afrika umeelezea "masikitiko makubwa" juu ya uamuzi wa Moscow wa kusitisha mpango wa mauzo ya nafaka.

Baadaye wiki hii Urusi itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa pili wa Russia-Afrika na Jukwaa la Kiuchumi na Kibinadamu la Russia-Afrika, kulingana na Kremlin.

Mashirika ya misaada ya kibinadamu yanasema Afrika inategemea pakubwa nafaka kutoka Urusi na Ukraine.

Mpango huo wa nafaka ulikuwa umewezesha mauzo ya nje ya zaidi ya tani milioni 32 za nafaka za Ukreni katika mwaka jana.

TRT World