Vikosi vya jeshi na polisi walizingira eneo hilo mara moja na walikuwa wakifanya uchunguzi wa awali na kuangalia kamera za usalama kwa dalili yoyote ya nani anaweza kutekeleza shambulio hilo. / Picha: Reuters

Mlipuko mkubwa unaoaminika kuwa wa bomu ulipiga Misa ya Kikatoliki na kuua watu wasiopungua wanne na kujeruhi wengine kadhaa huko Mindanao, Kusini mwa Ufilipino, maafisa wamesema.

Misa ya asubuhi ilikuwa ikiendelea Jumapili katika ukumbi wa mazoezi katika chuo kikuu cha Jimbo la Mindanao, jiji la Marawi wakati mlipuko huo ulipotokea.

Mlipuko huo umesababisha hofu kati ya wanafunzi na walimu na kuwaacha wahasiriwa wakivuja damu na kutapkaa kil asehemu, alisema Taha Mandangan, mkuu wa usalama wa chuo hicho kinachoendeshwa na serikali.

Angalau wawili kati ya waliojeruhiwa walikuwa katika hali mahututi, Mandangan alisema.

"Ni wazi hiki ni kitendo cha ugaidi. Sio ugomvi rahisi kati ya watu wawili. Bomu litaua takriban kila mtu, " Mandangan alisema.

Kamanda wa jeshi la mkoa huo, Meja Jenerali Gabriel Viray III, alisema watu wasiopungua wanne waliuawa kwenye mlipuko huo, wakiwemo wanawake watatu.

Wengine wafikao 50 walikimbizwa hospitali mbili kwa ajili ya matibabu ya majeraha madogo.

Ni wawili tu kati ya waliouawa waliotambuliwa, maafisa walisema.

Vikosi vya jeshi na polisi walizingira eneo hilo mara moja na walikuwa wakifanya uchunguzi wa awali na kuangalia kamera za usalama kwa dalili yoyote ya nani anaweza kutekeleza shambulio hilo.

Mlipuko huo wa mauti ulianzisha kengele ya ulinzi nje ya jiji la Marawi wakati msimu wa Krismasi ulipoanzisha kipindi cha kusafiri, ununuzi na msongamano wa magari kote nchini.

Kufuatia shambulio hilo linaloshukiwa la bomu, walinzi wa pwani wa Ufilipino walisema kuwa waliwaamuru wafanyakazi wake wote kuimarisha ukusanyaji habari za kijasusi, kufanya ukaguzi mkali wa vivuko vya abiria na kupelekwa kwa mbwa wa kunusa mabomu na maofisa wa baharini.

"Katikati ya kitendo hiki cha kinyama, huduma bora ya umma lazima ishinde," Mkuu wa walinzi wa pwani Admiral Ronnie Gavan alisema katika taarifa.

Shambulio la kutisha

Mshauri wa rais Carlito Galvez, ambaye alikuwa mkuu wa jeshi na sasa anasimamia jitihada za serikali za kukomesha uasi, alilaani vikali kile alichokiita tukio la mabomu.

"Shambulio hili la kutisha, lililotokea wakati wa Misa, linaonyesha njia zisizo na huruma ambazo vitu hivi visivyo na sheria vitatumiwa kuzua hofu, hasira na uadui kati ya watu wetu, " Galvez alisema katika taarifa. "Hatutaruhusu hii kutokea.”

Kufikia sasa, hakuna dalili za wazi za ni nani aliyehusika na mlipuko huo, lakini polisi walisema wataangalia uwezekano wa kuhusika kwa wanamgambo, ambao bado wana uwepo katika eneo hilo licha ya miaka ya mashambulizi ya kijeshi na polisi.

Mkurugenzi wa polisi wa mkoa huo Brig. Jenerali Al Lan Nobleza alisema wachunguzi walikuwa wakitathmini ikiwa mlipuko huo ulisababishwa na bomu la kujitengenezea nyumbani au bomu la kurushwa kwa mkono.

Aidha, wachunguzi wanatathmini pia ikiwa shambulio hilo lilikuwa na uhusiano na mauaji ya wanamgambo 11 wanaoshukiwa katika shambulio la kijeshi lililoungwa mkono na mashambulio ya angani na moto wa silaha ijumaa karibu na mji wa Datu Hoffer kusini mwa Mkoa wa Maguindanao.

Nobleza alisema kuwa wanamgambo waliouawa ni wa Dawlah Islamiyah, kundi lenye silaha ambalo lilikuwa limejiunga na Daesh na bado lina uwepo Katika mkoa wa Lanao Del Sur, ambapo mji wa Marawi unapatikana.

AP