Waziri mmoja wa baraza la mawaziri la Israel alizuiwa kuingia katika lango la wageni katika hospitali. Walinzi wa mwingine walimwagiwa kahawa na mmoja wa familia waliofiwa. Wa tatu alirushiwa matusi ya kuwa "msaliti" na "mpumbavu" alipofokewa alipokuja kuzifariji familia zilizohamishwa wakati wa hofu.
Shambulio la Oktoba 7 lililofanywa na wapiganaji wa Hamas limewafanya Waisraeli kuaminiana. Lakini kuna upendo mdogo unaoonyeshwa kwa serikali inayoshutumiwa sana kwa kuacha ulinzi wa nchi hiyo na kuiingiza katika vita vya Gaza ambavyo vinasumbua eneo hilo.
Chochote kitakachotokea wakati Israel ikiendelea na mashambulizi yake mabaya dhidi ya Gaza iliyozingirwa, siku ya hukumu inakaribia kwa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, baada ya juhudi za muda mrefu za kujikomboa kisiasa.
Kujipa ujabari kwa Netanyahu kumezidisha hasira za umma juu ya vifo 1,300 vya Israeli kama mwanamkakati mfano wa Churchillian kuwa anaweza kutabiri vitisho vya usalama wa kitaifa.
Hali nyingine ni mgawanyiko wa kijamii mwaka huu kutokana na harakati ya muungano wake wa kidini na wenye msimamo mkali wa kurekebisha mahakama, ambayo ilisababisha kuondoka kwa baadhi ya askari wa akiba na kuzua mashaka - ambayo sasa yamesababisha kumwaika damu, wengine wanabishana - kuhusu utayari wa vita.
"Fedheha ya Oktoba 2023" ilikuwa kichwa cha habari katika gazeti lililokuwa likiuzwa zaidi kila siku Yedioth Ahronoth, lugha iliyokusudiwa kukumbuka kushindwa kwa Israel kutarajia mashambulizi pacha ya Misri na Syria mnamo Oktoba 1973, ambayo hatimaye ilisababisha waziri mkuu wa wakati huo Golda Meir kujiuzulu.
Amotz Asa-El, mtafiti mkuu katika Taasisi ya Shalom Hartman huko Jerusalem, alitabiri hatima sawa ya Netanyahu na chama chake kikuu cha muda mrefu, cha kihafidhina cha Likud.
"Haijalishi kama kuna tume ya uchunguzi au la, au kama anakiri kosa au la. Kilicho muhimu ni kile 'Waisraeli wa kati' wanafikiria - ambayo ni kwamba huu ni uzembe na kwamba waziri mkuu anawajibika," Asa-El aliliambia shirika la habari la Reuters.
"Atakwenda, na mfumo wake mzima wa utawala pamoja naye."
Kura ya maoni katika gazeti la Maariv iligundua kuwa asilimia 21 ya Waisraeli wanataka Netanyahu abakie waziri mkuu baada ya vita.
Asilimia 66 walisema "mtu mwingine", na asilimia 13 walikuwa hawajaamua.
Baraza la mawaziri la vita vya dharura
Lakini Waisraeli sasa hawataki kura. Wanataka hatua zichukuliwe, na huku vita vya Israel dhidi ya Gaza vikizidi kuongezeka katika uwezekano wa uvamizi wa ardhini, Gantz, mkuu wa zamani wa kijeshi, ameweka kando tofauti za kisiasa kuungana na Netanyahu katika baraza la mawaziri la dharura.
Akiwa na shughuli nyingi na wajumbe wakuu na wajumbe wa kigeni, Netanyahu amepunguza mawasiliano yake na umma.
Alikutana na jamaa wa wafungwa wapatao 200 waliokuwa wakizuiliwa huko Gaza, bila kamera za televisheni kuwepo.
Huku kukiwa na kilio kikubwa, mke wake alitembelea familia moja kwa huzuni.
Netanyahu pia bado hajatoa kauli zozote za uwajibikaji binafsi - licha ya kuwa jenerali wake mkuu, waziri wa ulinzi, mshauri wa usalama wa taifa, waziri wa mambo ya nje, waziri wa fedha, na wakuu wa kijasusi wote kushindwa kutarajia na kuzuia uvamizi wa kushtukiza wa Hamas.
Israel imefanikiwa kupata uungwaji mkono wa mataifa ya Magharibi kwa vita vyake. Hilo linaweza kutoweka ikiwa uvamizi wa ardhini wa Gaza utasababisha kuongezeka kwa vifo vya Wapalestina na hasara za kijeshi.
Vita hivyo vinaweza pia kuvunja mafanikio mawili ya sera ya kigeni ya Netanyahu: amani na Saudi Arabia, ambayo sasa imesitishwa, na kuizuia Iran.
Wapangaji wa kijeshi wanasema vita vya Gaza, ambavyo lengo lake lililotajwa ni kuangamizwa kwa Hamas, vinaweza kudumu miezi kadhaa.
Netanyahu angefurahia mapatano ya kisiasa kwa muda huo, Asa-El alisema.
Ikiwa afya ya waziri mkuu itamudu ni swali lingine.
Mnamo Julai, aliwekwa kifaa cha kudhibiti moyo wakati maandamano ya mahakama yalipoongezeka. Atatimiza miaka 74 siku ya Jumamosi.
Baadhi ya wafafanuzi wamependekeza kwamba mifarakano ndani ya jamii ya Israel, na kiwango ambacho walidhoofisha usalama wa taifa, inapaswa kuwajibishwa watu zaidi kuliko Netanyahu pekee.
"Tulisahau kuwa ndugu, na tukapata vita," Amit Segal, mchambuzi wa kisiasa wa kituo cha runinga cha Channel 12, alisema kwenye Telegram.
"Hujachelewa kurekebisha. Acha ugomvi - sasa."
Akitaja dharau iliyoletwa kwa baadhi ya mawaziri, Asa-El alisema mifarakano inaonekana tayari kujitokeza ndani ya muungano wa serikali.
"Unasikia watu mitaani ambao ni wafuasi wa asili wa Likud wakizungumza juu yao kwa uhasama usio na shaka," alisema.
"Ghadhabu itazidi kukua, na juhudi hii inayoonekana ya Netanyahu kukwepa wajibu wake mwenyewe inawafanya watu kukasirika zaidi. Hawezi tu kukubali kusema: 'Tumejidanganya."