Wapiganaji wa Wagner walitumwa Rostov-on-Don / Picha: Reuters

Rais wa Urusi Vladimir Putin alimshutumu mkuu wa kikundi cha mamluki cha Wagner, Yevgeny Prigozhin kwa "uhaini" baada ya wapiganaji wa Ukraine kuvuka na kuingia katika mji wa Rostov nchini Urusi mapema Jumamosi.

Kikundi cha Wagner ni kampuni ya kibinafsi ya kijeshi iliyoundwa 2014 na Prigozhin,

Mvutano kati ya Moscow na kundi hilo uliongezeka baada ya Prigozhin kushutumu vikosi vya Urusi kwa kushambulia wapiganaji wake.

Rais Putin sasa ametaka tofauti zozote kati ya Wagner na Urusi ziondolewe akitoa uhakikisho wa usalama kwa mamluki wa Wagner, ambao anasema wanapaswa kuacha kufanya uasi dhidi ya uongozi wa kijeshi wa Moscow.

"Tunawaomba wapiganaji wa kikosi cha mashambulizi cha PMC Wagner. Mlidanganywa na kuwa waasi ," jeshi lilisema katika taarifa yake.

Alitoa wito kwa wapiganaji hao kuomba msaada ili kurejea katika maeneo yao ya kutoa huduma za usalama.

Rais Putin amesema wapiganaji hao wanawasaliti wananchi wa Urusi.

Kiev ilisema matukio "yanaanza tu" nchini Urusi, wakati mamluki wa Urusi Wagner walivuka kutoka Ukraine hadi Urusi ili kufanya uasi. Hii imefanyika miezi 16 baada ya uvamizi wa Kremlin nchini Ukraine.

"Kila kitu kinaanza tu nchini Urusi. Mgawanyiko kati ya wasomi ni dhahiri sana. Kukubaliana na kujifanya kuwa kila kitu kimetatuliwa haitafanya kazi," msaidizi wa rais wa Ukraine, Mykhailo Podolyak, alisema kwenye mtandawo wa Twitter.

Wizara ya Ulinzi ya Uingereza inasema maendeleo hayo mapya yanaashiria changamoto kubwa zaidi kwa taifa la Urusi katika siku za hivi karibuni.

TRT Afrika