Uvumbuzi wa kwanza ni katika eneo la mafuta la Ghadames, uliofanywa kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya uzalishaji na kampuni ya nishati inayomilikiwa na serikali ya Algeria ya Sonatrach, inayoonyesha viwango vya uzalishaji vya futi za ujazo milioni 13 za gesi na mapipa 327 ya ‘condensate’ kila siku, NOC ilisema.
Uvumbuzi wa pili wa gesi ulifanywa na Eni North Africa ya Italia, ambapo vipimo viwili tofauti vilionyesha viwango vya mtiririko wa futi milioni 14 na futi milioni 24. Uvumbuzi huu uko katika eneo la pwani magharibi mwa Libya.
NOC pia ilipata uvumbuzi pamoja na tawi la Repsol Libya, REMSA, la Hispania kwenye visima vya uchunguzi katika eneo la mafuta Murzuq, takriban kilomita 800 kusini mwa Tripoli. Vipimo baada ya kuchimba visima vilionyesha kiwango cha uzalishaji cha mapipa 763 ya mafuta kwa siku.
Uchumi wa Libya unategemea mafuta kwa zaidi ya asilimia 95 ya pato lake la kiuchumi, jambo linalofanya uvumbuzi huu kuwa muhimu sana kwa ukuaji wa taifa na sekta ya nishati.














