| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Ajali ya ndege yaua 14 nchini Sudan Kusini
Ndege hiyo, aina ya Cessna inadaiwa kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba, saa moja na robo asubuhi na kudondoka umbali wa kilomita 20, toka jiji la Juba, kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama wa Anga ya nchi hiyo.
Ajali ya ndege yaua 14 nchini Sudan Kusini
Ndege hiyo, aina ya Cessna inadaiwa kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba./Picha:Wengine

Watu wapatao 14, wamefariki dunia siku ya Jumatatu kufuatia ajali ya ndege ndogo karibu na mji mkuu wa Juba, Sudan Kusini.

Ndege hiyo, aina ya Cessna inadaiwa kuruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Juba majira ya saa moja na robo asubuhi na kudondoka umbali wa kilomita 20, toka jiji la Juba, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Usalama wa Anga ya nchi hiyo.

Taarifa za awali, zinaonesha kuwa ajali hiyo ilisababishwa na hali mbaya ya hewa iliyopelekea uoni hafifu kwa rubani wa ndege hiyo.

Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni raia 12 wa Sudan Kusini na Wakenya wawili.

"Miili ya waathirika iliungua vibaya,” alisema mmoja ya waokozi kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa.

Januari mwaka jana, watu 20 walipoteza maisha katika ajali ya ndege iliyotokea kaskazini mwa nchi hiyo.

Mwaka 2021, watu watano walifariki dunia baada ya ndege iliyokuwa mafuta kwa ajili ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kuanguka.

 

CHANZO:AFP
Soma zaidi
Rais wa Afrika Kusini aagiza hatua za kuwalinda wanawake kufuatia mfululizo wa mauaji
Misri yakana kuingilia mambo ya ndani ya Ethiopia na kuunga mkono makundi yenye silaha
Edward Kijanangoma atawazwa mfalme mpya wa Tooro
Je, Afrika itapata viti vya kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa?
Jeshi la Polisi Tanzania laonya wanaochochea mgomo wa madereva wa mabasi
Madaktari bingwa wa Tanzania waweka kambi ya matibabu Malawi
Makamu wa Rais Tanzania ataka vijana kupewa fursa za mafunzo ya ajira
Jeshi la Sudan lapinga madai ya kuunga mkono makundi ya upinzani Ethiopia
Uchaguzi Mkuu kurejesha utulivu Sudan Kusini?
Marekani italazimika kuondoka Mashariki ya Kati: Iran
Mashambulizi ya kigaidi mjini Mogadishu yapungua kwa karibu asilimia 90: Serikali ya Somalia
Maambukizi ya Ebola nchini DRC ni zaidi ya 8,000 tangu kuanza kwa mlipuko huo
Watoto 17 miongoni mwa wahamiaji 250 waliookolewa katika pwani ya Mauritania
Marekani kusitisha ufadhili wa sekta ya afya nchini Zimbabwe kufikia mwishoni mwa mwezi wa Septemba
Mwanamke wa kumi apatikana amefariki katika msururu  wa mauaji nchini Afrika Kusini
Qatar Airways yakopesha marubani kwa shirika la ndege la taifa la Rwanda
Wapiganaji wa RSF wahamia upande wa jeshi la Sudan baada ya kushuhudia 'maafa'
Mkuu wa Umoja wa Mataifa asikitishwa kwa kunyimwa viza  kiongozi wa Sudan, Burhan kuhudhuria UNGA
Jenerali wa DR Congo miongoni mwa watu 13 waliofariki katika ajali ya ndege
Afrika itapata hadhi ya uwanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa?