| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Korea Kusini yalaani mashambulizi ya meli Mlangoni Hormuz
Siku ya Jumapili, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ilisema kuwa mashambulizi kadhaa yalisababisha mlipuko kwenye meli ya HMM Namu inayosimamiwa na kampuni ya meli ya Korea (HMMCo).
Korea Kusini yalaani mashambulizi ya meli Mlangoni Hormuz
Meli ya Korea Kusini iliyoshambuliwa./Picha:Wengine

Korea Kusini imelaani vikali mashambulizi ya meli za kiraia katika eneo la Mlango Bahari wa Hormuz.

"Ni imani yetu kuwa mashambulizi haya hayawezi kuhahalishwa kwa njia yoyote ile,” alisema Mshauri wa Usalama wa Taifa la Korea Kusini, Wi Sung-lac.

Siku ya Jumapili, Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo ilisema kuwa mashambulizi kadhaa yalisababisha mlipuko kwenye meli ya HMM Namu inayosimamiwa na kampuni ya meli ya Korea (HMMCo).

“Tunajaribu kumtafuta aliyehusika na tukio hilo na vifaa vipi vilitumika katika kutekeleza shambulio hilo” alieleza," Wi.

CHANZO:AA