| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Uturuki na Algeria wasisitiza ushirikiano wa kimkakati wakati wa mkutano wa Erdogan-Tebboune
Uturuki na Algeria wameeleza dhamira ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kufuatia mkutano kati ya Marais Recep Tayyip Erdogan na Abdelmadjid Tebboune siku ya Alhamisi.
Uturuki na Algeria wasisitiza ushirikiano wa kimkakati wakati wa mkutano wa Erdogan-Tebboune
Rais wa Algeria Abdelmadjid Tebboune alianza ziara rasmi ya siku tatu nchini Uturuki Mei 6, 2026. / Reuters

Uturuki na Algeria wameeleza dhamira ya kuimarisha ushirikiano wa kimkakati kufuatia mkutano kati ya Marais Recep Tayyip Erdogan na Abdelmadjid Tebboune, katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, siku ya Alhamisi.

Ushirikiano ni katika sekta muhimu, ikiwemo nishati, madini, usafiri na kilimo.

Viongozi hao wawili pia walijadili uhusiano wa mataifa mawili na masuala ya kikanda wakati wa mkutano katika Ikulu ya Rais wa Uturuki.

Rais Erdogan aliielezea Algeria kama mmoja ya mshirika mkuu wa kibiashara wa Uturuki barani Afrika na akasisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirkiano wa kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.

"Tumedhamiria kuimarisha ushirikiano wetu na Algeria, ambayo ni moja ya washirika wetu wakuu kibiashara barani Afrika, katika maeneo mengi ya kimkakati, ikiwemo nishati, madini , usafiri na kilimo," Rais Erdogan alisema.

'Historia ya pamoja'

Aliongeza kuwa Uturuki na Algeria zimeongeza juhudi ya kufikia lengo la biashara kwa nchi hizo mbili la Dola bilioni $10, ambalo lilitangazwa kwa mara ya kwanza 2023.

Akieleza msingi wa kihistoria wa uhusiano wa Uturuki na Algeria, Erdogan alisema ushirikiano kati ya nchi hizo mbili unazingatia "kuheshimiana na upendo kutokana na historia ya pamoja."

"Ari ya umoja iko wazi siyo tu kwa uhusiano wa mataifa yetu, lakini kwa misimamo yetu ya pamoja tunayoionesha katika masuala mengi ya kimataifa," alisema.

Mkutano huo kati ya marais hao wawili ulisisitiza kuimarika kwa uhusiano kati ya Uturuki na Algeria huku Uturuki ikiendelea kuimarisha ushirikiano wake wa kidiplomasia na kiuchumi barani Afrika.

Rais Tebboune yuko nchini Uturuki kwa ziara rasmi ya siku tatu kuanzia Mei 6 hadi 8, 2026 kwa mualiko wa Rais Erdogan.

CHANZO:TRT Afrika