| Swahili
AFRIKA
2 dk kusoma
Wanafunzi 16 Kenya wafariki kufuatia ajali ya moto katika bweni la shule ya wasichana
Jumla ya wanafunzi 16 wamefariki katika ajali ya moto na wengine 74 wamejeruhiwa katika bweni la shule ya wasichana ya Utumishi Academy huko Gilgil, Kaunti ya Nakuru, Kenya, mapema alfajiri ya Alhamisi, jeshi la Polisi nchini Kenya limesema.
Wanafunzi 16 Kenya wafariki kufuatia ajali ya moto katika bweni la shule ya wasichana
Vikosi vya dharura vimewasili katika eneo la shule kuudhibiti moto na kuwasaidia wanafunzi walioathirika. / / Wengine

Jumla ya wanafunzi 16 wamefariki katika ajali ya moto na wengine 74 wamejeruhiwa katika bweni la shule ya wasichana ya Utumishi Academy huko Gilgil, Kaunti ya Nakuru, Kenya, mapema alfajiri ya Alhamisi, jeshi la Polisi nchini Kenya limesema.

Hali hiyo imesababisha hofu kubwa miongoni mwa wazazi, walimu na wakazi waliokusanyika nje ya shule hiyo.

Ripoti zinaonyesha kuwa moto huo ulianza majira ya saa saba usiku, ingawa Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limesema tukio hilo liliripotiwa rasmi majira ya saa tisa na nusu alfajiri, huku vikosi vya dharura vikiwahi kufika katika eneo la shule kuudhibiti moto na kuwasaidia wanafunzi walioathirika.

“Kufuatia tukio la moto lililoripotiwa majira ya saa 3:30 asubuhi katika shule ya Utumishi Girls Academy, Kaunti ya Nakuru, Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya limeanza kusaidia juhudi za kukabiliana na dharura hiyo,” ilisema taarifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu Kenya.

Shirika hilo limesema kuwa wataalamu wa kutoa usaidizi wa kisaikolojia wamewasili shuleni humo kuwasaidia wanafunzi, wazazi na walimu waliopata mshtuko huo.

“Wahudumu wetu wa kutoa huduma za kwanza za dharura, wahudumu wa ambulansi pamoja na wataalamu wetu wa usaidizi wa kisaikolojia kwa sasa wako eneo la tukio wakiwasaidia wanafunzi walioathirika kwa kushirikiana na wahudumu wengine pamoja na mamlaka husika,” ilisema Kenya Red Cross.

Maafisa wa polisi pamoja na wachunguzi kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) walipelekwa shuleni humo mara moja baada ya tukio hilo, huku mamlaka zikianza kuhesabu wanafunzi waliokuwepo wakati wa moto huo.

Jumla ya wanafunzi 16 wamefariki katika ajali ya moto na wengine 74 wamejeruhiwa katika bweni la shule ya wasichana ya Utumishi Academy huko Gilgil, Kaunti ya Nakuru, Kenya, mapema alfajiri ya Alhamisi, jeshi la Polisi nchini Kenya limesema.

CHANZO:TRT Afrika