| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Polisi Afrika Kusini wakamata dawa za kulevya za dola milioni 61 ndani ya lori kutoka Malawi
Katika miaka miwili iliopita, kumekuwa na matukio yasiopungua manne ya kufichua maabara za kutengeneza dawa nchini Afrika Kusini.
Polisi Afrika Kusini wakamata dawa za kulevya za dola milioni 61 ndani ya lori kutoka Malawi
Polisi wanachunguza uhusiano wa waliokamatwa na magenge ya dawa za kulevya Marekani ya Kusini. / Polisi wa Afrika Kusini

Polisi wa Afrika Kusini wa ulinzi wa mpakani wamesimamisha lori lililokuwa linatoka Malawi na kuelekea nchini humo likiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya karibu rand bilioni moja (Dola milioni 61), mamlaka zimesema siku ya Alhamisi.

Katika msako wa saa nane, maafisa wa usalama waligundua zaidi ya kilo 700 za methaqualone, ambazo zinatumiwa katika dawa ya Mandrax, mamlaka za mpakani zilisema.

Makadirio ya thamani yake inasemekana kuwa karibu rand bilioni moja, taarifa hiyo ilisema.

Rais wawili wa Malawi na mmoja wa Zambia walikamatwa, msemaji aliiambia AFP.

Uchunguzi unaendelea

Huku kukiwa na soko kubwa la mandrax nchini Afrika Kusini, taarifa hiyo inasema uchunguzi unaendelea kutathmini "dawa hizo zilikuwa zinapelekwa wapi na kama kundi hilo ni sehemu ya mtandao mkubwa wa wahalifu katika bara au duniani".

Katika miaka miwili iliopita, kumekuwa na matukio yasiopungua manne ya kufichua maabara za kutengeneza dawa nchini Afrika Kusini, yanayohusisha raia wa Mexico, kuzua wasiwasi kuwa magenge ya Mexico yanajaribu kuweka mizizi yake katika kanda.

CHANZO:TRT Afrika and agencies