Wabunge wa Tanzania wameeleza msimamo wao bungeni wakisisitiza kuwa nchi hiyo ni huru na inatakiwa kuheshimiwa katika masuala ya uhusiano wa kimataifa, kufuatia kauli za baadhi ya wabunge wa Marekani zilizoibua wasiwasi kuhusu hali ya uhuru wa kisiasa na haki za kiraia nchini.
Akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje, mbunge wa Mtama, Nape Nnauye, amesema Tanzania haiwezi kupimwa au kudhalilishwa kwa kutumia changamoto zake za ndani, bali inatakiwa kuendeleza ushirikiano wa kimataifa kwa misingi ya kuheshimiana.
Naye mbunge wa Tunduru Kaskazini, Ado Shaibu, ameunga mkono msimamo wa kulinda maslahi ya taifa, huku akiibua mjadala kuhusu uraia pacha, akitaka tafakuri mpya iwapo hofu iliyopo ni ya msingi au ni mtazamo unaohitaji kuangaliwa tena.
Mjadala huo umeibuka baada ya kauli za wabunge wa Marekani kupendekeza kutafakari upya uhusiano wao na Tanzania, hatua iliyochochea mjadala zaidi kuhusu nafasi ya Tanzania katika diplomasia ya kimataifa.
AFRIKA
1 dk kusoma
Wabunge Tanzania wataka taifa kuheshimiwa kufuatia kauli za Marekani
Mjadala huo umeibuka baada ya kauli za wabunge wa Marekani kupendekeza kutafakari upya uhusiano wao na Tanzania
Soma zaidi










