| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mamilioni ya mahujaji watekeleza nguzo muhimu ya Arafah
Hajj ni miongozi mwa nguzo tano za dini ya Kiislamu, kila Muislamu mwenye uwezo wa kifedha na afya anapaswa kutekeleza ibada hio angalau mara moja katika maisha yake.
Mamilioni ya mahujaji watekeleza nguzo muhimu ya Arafah
Mmamilioni ya mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanasimama sehemu moja, ambayo ni uwanja wa Arafah. / Reuters

Leo, mamilioni ya mahujaji kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wanasimama sehemu moja, ambayo ni uwanja wa Arafah.

Kitendo hiki ni muhimu sana katika ibada ya hajj, na huitwa "nguzo kuu ya Hajj" kwa sababu ibada hiyo haikamiliki bila ya Arafah.

Kwa kawaida, mahujaji huanza kusimama Arafah baada ya adhuhuri (Dhuhr) siku ya 9 Dhul Hijjah, na hubaki mpaka jua linapozama (Maghrib) siku hiyo hiyo.

Kutokana na mafundisho ya dini ya Kiislamu, siku hii imejaa rehema, na msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu, na ndio maana,  Waislamu duniani kote hata wale ambao hawakupata fursa ya kwenda kuhiji,  huzidisha ibada na kumuomba Mwenyezi Mungu.

Kwa wale ambao hawako Hijja, kufunga siku ya Arafah ni Sunna yenye malipo makubwa. Mtume Muhammad (SAW) alisema kuwa kufunga siku hii kunafutia madhambi ya mwaka uliopita na mwaka unaofuata.

Baada ya siku ya Arafah, inayofuata huwa ni Sikukuu ya Eid al-Adha ambayo ni Sikukuu ya kuchinja nakutoa sadaka ya nyama kwa mwenye uwezo, ikiwa ni njia moja wapo ya kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu.

CHANZO:TRT Afrika