| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Bunge la Senegal lamchagua aliyekuwa Waziri Mkuu Sonko kuwa spika mpya
Bunge la Senegal limemchagua aliyekuwa waziri mkuu kuwa spika
Bunge la Senegal lamchagua aliyekuwa Waziri Mkuu Sonko kuwa spika mpya
Ousmane Sonko alifutwa kutoka kwenye wadhifa wake wa Waziri Mkuu siku ya Ijumaa. / Anadolu Agency

Bunge la Senegal limemchagua aliyekuwa Waziri Mkuu Ousmane Sonko kuwa spika siku ya Jumanne, hatua ambayo itampa uwezo wa kuwa mpinzani wa Rais Bassirou Diomaye Faye.

Spika wa bunge El Malick Ndiaye alijiuzulu siku ya Jumapili hatua ambayo wachambuzi wanasema ilikuwa ya wazi ya kumpa Ousmane Sonko nafasi kuwania uongozi wa bunge, ambapo chama chake cha Pastef kina wabunge wengi.

Wabunge walitakiwa kurudi kwa kikao kamili siku ya Jumanne, ambapo Sonko alirudishwa kama mbunge na baadaye kuchaguliwa spika wa bunge hilo.

Hata hivyo, upinzani nchini Senegal ulisusia kikao hicho.

Rais Faye alimfuta kazi Sonko siku ya Ijumaa na kuvunja serikali. Amemteua mwanauchumi Ahmadou Al Aminou Lo kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo siku ya Jumatatu.

Uamuzi wa rais unakuja baada ya miezi kadhaa ya vuta nikuvute ya kisiasa na Sonko, aliyekuwa mshirika wake wa karibu, ambaye kwa kumuunga mkono kwake ndiko kulifanikisha yeye kuingia madarakani baada ya kukishinda chama tawala 2024.

CHANZO:TRT Afrika and agencies