| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Zaidi ya watengeneza maudhui 200 wa Afrika wakutana Ethiopia
Mbali na kujenga mahusiano ya kikazi, mkutano huo unalenga kushirikiana katika kutengeneza maudhui na kuielezea taswira halisi ya bara la Afrika duniani.
Zaidi ya watengeneza maudhui 200 wa Afrika  wakutana Ethiopia
Watengeneza maudhui wanaoshiriki mkutano huo./Picha:EBC / Others

Watengeneza maudhui kutoka nchi mbalimbali Afrika, wanakutana jijini Addis Ababa Ethiopia kwa ajili ya mkutano wa kwanza wa African Social Media Influencer Summit (ASMIS) 2026.

Mkutano huo wa siku mbili, umewakutanisha pamoja watengeneza maudhui, wacheshi na watu maarufu wa mitandaoni kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Tanzania, Botswana, Sierra Leone na Eswatini.

Mbali na kujenga mahusiano ya kikazi, mkutano huo unalenga kushirikiana katika kutengeneza maudhui na kubadilisha taswira ya Afrika duniani.

Dhima mbalimbali zitatawala mkutano huo, zikiwemo uchumi wa watengeneza maudhui, utengenezaji fedha kwa njia za maudhui na matumizi ya mitandao ya kijamii kuelezea simulizi za Afrika.

Mkutano huo umevutia mashabiki wengi mitandaoni na kuonyesha jinsi watengeneza maudhui wa Afrika Mashariki wanavyozidi kupata nafasi kwenye jukwaa la kimataifa.

Kati ya wanaohudhuria mkutano huo, ni pamoja na Mtanzania Fanuel John Masamaki maarufu kama Zerobrainer ambaye alipata wasaa wa kucheza mpira pamoja na mtengeneza maudhui wa Botswana, William Last KRM.

CHANZO:TRT Afrika Swahili