| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Rais wa Uturuki, Makamu wa Rais wa China wajadili uhusiano wa nchi hizo mbili
Rais wa Uturuki, ametoa wito wa kuimarishwa kwa ushirikiano kati ya nchi yake na China katika sekta za uwekezaji, nishati, biashara na utalii, akisema kuwa njia ya 'Middle Corridor' inaweza kuunganishwa na Mpango wa China Belt and Road.
Rais wa Uturuki, Makamu wa Rais wa China wajadili uhusiano wa nchi hizo mbili
Erdogan alielezea azma ya Uturuki ya kuchukua hatua zinazohitajika ili kuimarisha ushirikiano. / / َAA

Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan, amekutana na Makamu wa Rais wa China, Han Zheng, katika jiji la Antalya, kusini mwa Uturuki, ambako viongozi hao wote wanahudhuria Mkutano wa Viongozi wa COP31, unaohusu Mabadiliko ya Tabianchi.

Kwa mujibu wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki, mkutano huo uliofanyika Jumatano ulijikita katika kujadili uhusiano wa nchi hizo mbili, pamoja na masuala ya kikanda na kimataifa.

Katika mazungumzo hayo, Erdogan alisisitiza umuhimu wa kuharakisha ushirikiano kati ya nchi hizo, akieleza kuwa kuna fursa ya kuimarisha uhusiano katika maeneo mbalimbali, hususan uwekezaji, nishati, biashara na utalii.

Aidha, Erdogan alieleza dhamira ya Uturuki ya kuchukua hatua zinazohitajika ili kuendeleza na kuimarisha ushirikiano huo.

Akizungumzia masuala ya miundombinu na biashara, Erdogan alisema kuwa njia ya ‘Middle Corridor’ inaweza kuoanisha na Mpango wa China wa ‘Belt and Road’.

Aliongeza kuwa uwezekano wa ushirikiano utakaotokana na kuzingatia mipango hiyo miwili kwa pamoja, sambamba na Mradi wa ‘Development Road’, unatoa fursa kubwa kwa nchi zote mbili.

CHANZO:AA