Mkuu wa Shirika la Ujasusi la Uturuki Ibrahim Kalin anasema hakuwezi kuwa na amani Mashariki ya Kati bila kushughulikia suala la Palestina na kumaliza ukaliaji wa Israel.
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la TRT World Forum 2026 siku ya Ijumaa katika Ukumbi wa Mkutano wa Istanbul, Kalin alisema:
“Hakuna Palestina bila Gaza, na hakuna amani Mashariki ya Kati bila amani kuhusu suala la Palestina.”
“Watu wa Palestina siyo tatizo; tatizo ni ukaliaji,” aliongeza, akisisitiza kuwa “bila kumaliza ukaliaji, hakutakuwa na suLuhu, hakuna amani, hakuna haki Mashariki ya Kati.”
Kalin alisema Gaza ni sehemu muhimu ya Palestina na mapambano ya Palestina ni zaidi ya suala la maeneo hadi kwa misingi ya haki na usawa.
“Gaza ni sehemu muhimu ya Palestina, na Palestina ni sehemu ya mapambano ya haki, heshima, na usawa kwa wote,” alisema.
“Siyo tu kuhusu sehemu ya ardhi; pia ni kuhusu misingi ya heshima duniani, uadilifu.”
Mapema, akizungumza katika jukwaa hilo, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan alisema kuwa matukio ya hivi karibuni katika kanda yanaonesha kuwa mfumo wa sasa wa kimataifa “unapeperusha bendera nyeupe ishara ya kusalimu amri,” akishtumu taasisi za dunia kwa kukaa kimya huku vurugu za Israel zikiendelea Gaza na Ukingo wa Magharibi uliokaliwa.





















