| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Afrika Kusini yasema matokeo ya nusu muhula Marekani yanaashiria mwanzo mpya
Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa siku ya Jumatano alisema matokeo ya uchaguzi wa nusu muhula Marekani yanaashiria mwanzo mpya katika uhusiano wa masuala ya dunia.
Afrika Kusini yasema matokeo ya nusu muhula Marekani yanaashiria mwanzo mpya
Rais wa Afrika Kusini anasema matokeo ya uchaguzi wa nusu muhula Marekani yanaashiria mwanzo mpya.

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa alisema siku ya Jumatano kuwa matokeo ya uchaguzi wa nusu muhula Marekani yanaashiria mwanzo mpya katika masuala ya dunia.

Uhusiano kati ya Afrika Kusini na Marekani si mzuri kwa sasa.

Wiki hii, serikali ya Trump imeondoa fursa ya Afrika Kusini kufikia soko la Marekani bila kodi, baada ya kusitisha msaada wa kifedha mwaka uliopita na kumfukuza balozi wake wa nchini Marekani.

Trump amekuwa akiishtumu nchi hiyo kwa kile alichokisema kuwa ni mateso kwa wazungu, jambo ambalo Afrika Kusini inasema ni uongo. .

Afrika Kusini kuondolewa katika AGOA

"Tumeona chama cha Democratic kimechukua udhibiti wa Seneti na Baraza la Wawakilishi, na watu wa Marekani wamezungumza. ... naamini huu utakuwa mwanzo mpya kwa masuala ya dunia," Ramaphosa aliwaambia waandishi wa habari baada ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaofanyika siku ya Jumatano.

CHANZO:TRT Afrika Swahili