| Swahili
UTURUKI
1 dk kusoma
Balozi wa Uturuki nchini Sudan Kusini Metin Ergin afariki dunia
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan ameongoza katika kumkumbuka mwanadiplomasia huyo aliefariki siku ya Jumatatu.
Balozi wa Uturuki nchini Sudan Kusini Metin Ergin afariki dunia
PICHA YA MAKTABA: Balozi wa Uturuki nchini Sudan Kusini Metin Ergin akiwa na Rais Salva Kiir katika ikulu ya rais mjini Juba.

Uturuki imekuwa ikimkumbuka Balozi wake wa Sudan Kusini, Metin Ergin, aliefariki dunia siku ya Jumatatu akiwa na umri wa miaka 59.

"Napenda kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia yake, wapendwa wake na jamii yetu, na tunaomba Mungu amrehemu Balozi Ergin, ambaye alitumikia nchi yetu kwa miaka 35 kwa dhati," Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Hakan Fidan alisema katika taarifa siku ya Jumanne.

Wizara ya Mambo ya Nje pia ilitoa salamu zake za rambirambi kufuatia kifo cha mwanadiplomasia huyo.

"Tunaskitika kutangaza kifo cha Novemba 2 2026 cha mwenzetu Metin Ergin (1967, Istanbul), ambaye amekuwa akifanya kazi katika Wizara yetu tangu 1992 na amewakilisha Taifa letu kama Balozi Mostar, Bosnia na Herzegovina na Antwerp, Ubelgiji, na kama Balozi nchini Sudan Kusini," wizara ilisema katika taarifa.

"Atazikwa katika makaburi ya Zincirlikuyu jijini Istanbul baada ya swala ya Ijumaa tarehe 6 Novemba 2026. Mungu ailaze roho yake pahali pema, na tunatoa salamu zetu za rambirambi kwa familia yake," iliongeza.

CHANZO:TRT Afrika English
Soma zaidi
Trump ampigia simu Erdogan, amtakia heri ya mkutano wa Kiturki
Uturuki yalenga kushirikiana na jumuiya ya Kiturki
Katika picha: Uturuki yaadhimisha miaka 103 ya Jamhuri
Uturuki yaadhimisha miaka 103 ya Siku ya Jamhuri kwa sherehe za kitaifa
“Uturuki ina nguvu zaidi leo kuliko jana,” asema Rais Erdogan katika maadhimisho ya Siku ya Jamhuri
Uturuki yasema ipo tayari kuingia mkataba wa majini na Misri
Erdogan ataka uongozi imara ndani ya Umoja wa Mataifa
Bunge la Uturuki lauidhinisha mkataba wa Makkah
Erdogan aapa kutetea haki za bahari za Uturuki, atoa wito wa umoja wa Libya
Biashara, ushirikiano wa anga kuwa sehemu ya ajenda ya mkutano wa nchi za Kiturki
Katika Siku ya UN, Erdogan wa Uturuki ataka Baraza la Usalama liwe 'la haki na shirikishi'
Ukiukaji wa Israel huko Gaza unadhoofisha imani katika mfumo wa kimataifa: Fidan
Uturuki yaandaa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa R4 kuhusu usalama wa kikanda
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki akutana na wenzake wa Uingereza na Pakistan
Erdogan aahidi kuendeleza diplomasia katika Kongamano la 9 la Upatanishi la Istanbul
Uturuki na Canada zalenga kuinua kiwango cha biashara hadi Dola bilioni 10
Rais Erdogan aipongeza Libya kwa kuidhinisha makubaliano ya mipaka ya bahari na Uturuki
Uturuki kudumisha uwepo wake wa kijeshi Syria na Iraq hadi usalama wa mipaka utakapoimarishwa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Fidan na mkuu wa NATO Rutte wajadili usalama wa Bahari Nyeusi
Erdogan: Uturuki imefanikiwa kutibua njama za kuitumbukiza katika vita vya kikanda