| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Mfanyakazi wa Marekani akiri kutoa siri za kijasusi kwa Ethiopia
Abraham Teklu Lemma, 54, alitoa siri za Marekani kwa maafisa waandamizi wa Ethiopia kwa zaidi ya miaka miwili, kulingana na ofisi ya mwanasheria mkuu.
Mfanyakazi wa Marekani akiri kutoa siri za kijasusi kwa Ethiopia
PICHA YA MAKTABA: Taarifa hizo za kijasusi zilitumiwa na maafisa wa Ethiopia katika oparesheni za kijeshi.

Mfanyakazi wa zamani wa serikali ya Marekani amekiri kuipa Ethiopia taarifa za kijasusi ambazo walitumia katika oparesheni za kijeshi, Wizara ya Haki ya Marekani ilisema siku ya Jumanne.

Abraham Teklu Lemma, 54, alitoa siri za Marekani kwa maafisa waandamizi wa Ethiopia kwa zaidi ya miaka miwili, kulingana na ofisi ya mwanasheria mkuu.

 Siku ya Jumanne, Lemma, alikiri kula njama ya kutoa taarifa za ulinzi kwa serikali ya kigeni.

 Alikuwa anafanya kazi kama mtaalamu wa kompyuta katika Wizara ya Haki, waendesha mashtaka walisema.

Jeshi la Ethiopia na idara ya ujasusi

Kulingana na waendesha mashtaka, taarifa hizo zilifikia jeshi la Ethiopia na idara ya ujasusi kati ya mwaka 2021 na Agosti 2023, alipokamatwa.

Waendesha mashtaka walieleza kuhusu ujumbe wa Disemba 2021 ambapo Lemma alimwambia mshirika wake wa Ethiopia wakabiliane vikali na wapinzani wa serikali.

Serikali ya Ethiopia haijazungumza lolote hadharani kuhusu kesi hiyo.

Afisa wa shirika la FBI la Marekani, Roman Rozhavsky, alisema Lemma alikiri kuwa maafisa wa Ethiopia walitumia taarifa za kijasusi alizowapa katika oparesheni za kijeshi.

Taarifa ya Wizara ya Haki haijaeleza wazi kuhusu oparesheni hizo mahsusi au kusema kama mtu yeyote aliuawa kutokana na ukiukwaji wa utaratibu wa kijasusi.

 

CHANZO:TRT Afrika Swahili