| Swahili
AFRIKA
1 dk kusoma
Sudan Kusini kuajiri maafisa 10,000 wa polisi kabla ya uchaguzi wao wa kwanza
Maafisa hao watapelekwa katika vituo vya usajili wa wapigaji kura na vya kupiga kura, pamoja na ulinzi,
Sudan Kusini kuajiri maafisa 10,000 wa polisi kabla ya uchaguzi wao wa kwanza
Sudan Kusini inakabiliwa na changamoto za kiuchumi na usalama.

Sudan Kusini inasema kuwa imeanza kuajiri maelfu ya maafisa wa polisi wakati ikijiandaa kwa uchaguzi wake wa kwanza mwezi Disemba.

Msemaji wa polisi Daniel Justin aliithibitishia AFP kuwa watu 10,000 wataajiriwa katika majimbo yote 10, ikiwemo 3,000 katika jimbo la Bahr El Ghazal Kaskazini na 1,200 katika jimbo la Equatoria ya kati.

Justin aliiambia AFP kuwa maafisa hao wataungana na wengine 70,000 kote nchini.

Nchi hiyo inakabiliwa na changamoto za kiuchumi na usalama.

Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika wameeleza wasiwasi wao kuhusu utayari wa nchi hiyo kwa ajili ya uchaguzi wa Disemba 22, lakini Rais Salva Kiir anaonekana kuwa na nia ya kuendelea kuwepo madarakani.

Msemaji wa polisi jimbo la Bahr El Ghazal Kaskazini Madut Ngong Aleu amesisitiza kuwa maafisa wapya watapelekwa kuhakikisha “usalama wakati wa uchaguzi ujao”.

Polisi watakuwepo katika vito vya kusajili wapiga kura na vya kupiga kura, pamoja na ulinzi, alisema.

Maafisa waliiambia AFP kuwa serikali inafadhili mpango huo, bila msaada kutoka nje, ingawa hawakutoa taarifa zaidi.

Sudan Kusini imepitia vurugu tangu kuwa taifa huru, ikiwemo vita vya wenyewe kwa wenyewe kati ya mwaka 2013 na 2018 ambavyo vilisababisha vifo vya watu karibu 400,000.

CHANZO:TRT Afrika Swahili