| Swahili
ULIMWENGU
1 dk kusoma
Mlipuko wa volcano waua 3 nchini Indonesia, wengine 20 hawajulikani walipo
Watu watatu wamefariki dunia kutokana na mlipuko wa volkano ya Mlima Dukono kwenye kisiwa cha Halmahera katika jimbo la North Maluku nchini Indonesia, huku wengine 20 hawajulikani walipo.
Mlipuko wa volcano waua 3 nchini Indonesia, wengine 20 hawajulikani walipo
Serikali ya Indonesia imesema imepeleka waokoaji ili kuwahamisha wapanda milima waliokwama kutokana na mlipuko huo./ / AA

Serikali ya Indonesia imesema imepeleka waokoaji ili kuwahamisha wapanda milima waliokwama kutokana na mlipuko huo.

Shirika la habari la Detik nchini humo limemnukuu Erlichson Pasaribu ambae ni afisa wa polisi akisema kuwa kati ya watu watatu waliofariki, mmoja ni raia wa kigeni.

Volkano hiyo ililipuka majira ya saa 1:41 usiku wa kuamkia Ijumaa (1041GMT Alhamisi), ikitoa wingu kubwa la moshi lililofika umbali wa takribani kilomita 10 angani.

Shirika la Kitaifa la Usimamizi wa Maafa la Indonesia (BNPB) lilisema: “Kuna taarifa za watalii wawili wanaoshukiwa kufariki katika tukio lililotokea eneo la Mlima Dukono.”