Mwanamke mmoja mjamzito kutoka Ghana aliyeingia Marekani akiwa na viza halali na mtoto wake wa miaka minne ambaye alitakiwa kutibiwa alizuiliwa katika kituo kisichokuwa na madirisha kwa wiki moja uwanja wa ndege wa Washington, mawakili walieleza mahakama.
Annabella Gyasi aliwasili siku ya Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dulles kwa ajili ya kuelekea kwa miadi na daktari ya mwanawe wa kiume, ambaye alizaliwa na matatizo ya mikono, katika hospitali ya Watoto ya Akron huko Ohio, kulingana na taarifa zilizowasilishwa na shirika la American Civil Liberties Union of Virginia.
Wawili hao walikuwa wamekwenda Marekani 2024 kwa ajili ya matibabu, mawakili wake walisema, lakini wakarudi Ghana baada ya kuambiwa kuwa mtoto alikuwa mdogo kufanyiwa upasuaji.
Alikuwa na tiketi ya Mei 30 kuunganisha safari hadi Akron, kuona kama mtoto amekuwa kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.
Badala yake, wote wakazuiwa katika kituo cha uhamiaji. Gyasi, 38, ana ujauzito wa zaidi kidogo ya miezi minne.
Walizuiliwa kinyume cha sheria
“Bi Gyasi alisafiri Marekani kwa njia halali ili mtoto wake apate matibabu, lakini kukamatwa kinyume cha sheria na mateso aliyopitia Dulles kunaweka afya ya mtoto wake na yeye mwenyewe katika hatari,” Sophia Gregg, mwanasheria mwandamizi wa haki za wahamiaji katika shirika la ACLU la Virginia, alisema katika taarifa.
Maafisa wa uhamiaji wamesisitiza kuwa hajateswa.
“Madai haya ni ya uongo," Wizara ya Mambo ya Ndani imesema katika taarifa. “Kila mtu aliye kizuizini, ikiwemo mtu huyu, anahudumiwa vizuri, ikiwemo kuangaliwa afya na daktari, matibabu, na chakula."
Tangu kuwasili Marekani, Gyasi amepelekwa hospitalini mara mbili kwa matatizo ya ujauzito.
Akihofia kuhusu mtoto wake aliye tumboni, Gyasi anasema afadhali arudishwa Ghana kuliko kuzuiliwa bila chakula cha kutosha.
Jaji Leonie Brinkema ameagiza kesi kusikilizwa siku ya Ijumaa.















